Hapa ni katika Kijiji cha Saranda,Mkoani Singida ambapo wananchi wa maeneo haya hufaidika sana pindi treni ya reli ya kati inapokuwa inapita katika eneo hilo kwani huwawezesha kuleta biashara zao hapo na kuziuza abiria wanaosafiri na treni hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Makutupora Mkoani Dodoma wakiwa na biarashara zao wakiwauzia wasafiri waliopanda treni ya reli ya kati,ambayo inabeba abiria waendao katika mikoa ya Kigoma,Mwanza na Mpanda.ni dhahiri kwamba Serikali inatakiwa kuonyesha juhudi kubwa kwa usafiri huu ili kuweza kusaidinia kupunguza makali ya ugumu wa maisha kwa wakazi wa maeneo mbali mbali hapa nchini.
Wakazi wengi wa maeneo haya ya vijijini ni Wakulima,hivyo wakati treni ikipita hapo na wao hulazimika kuacha kilimo kwa muda na kuja kuuza bidhaa zao mbali mbali.
Mwanamama na mwanae mgongoni akiwa na bidhaa zake akitafuta wateja wa kununua.
Kuku wa kienyeji ni wengi sana katika vijiji hivi vya njiani (ila utaratibu wa ubebaji ndio hauzingatiwi kabisa).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Hivi ni Kijiji cha Saranga au Saranda?

    ReplyDelete
  2. Hamna video ya kuonyesha usafiri wa reli ya kati ili pamoja na wale wasafiri wa kawaida lakini inawezekana kupata watalii wa ndani na nje kufaidi uhondo wa kusafiri na treni reli ya kati.
    Video tafadhali.
    Mdau
    Mtalli toka ngambo.

    ReplyDelete
  3. Pamoja na kurudishwa huduma hizi za reli ambazo zilidumu kwa miaka mingi, tujulishwe kwa nini huduma hizi zilikufa. Wananchi wengi sana wameathirika hasa kiuchumi kutokana na huduma hizi kusitishwa. Vilevile tungependa kujua ni lini huduma toka Dar, Tanga Moshi zitarejeshwa?

    ReplyDelete
  4. Ama kweli Ukanda wa Reli, maisha bila ya reli haiwezekani!

    Hivi tujiulize,m kwa muda wote ambao Treni ilisimamisha huduma hawa ndugu zetu waliishi namna gani, ikiwa maisha yao yanategemea kuimarika kwa safari za reli?

    Ni wazi ya kuwa walikuwa Gizani, kiza kilitanda na walikuwa hawana pa kushika!

    Ni wazi utakuta mtu alikopa hadi akawa anakwepwa na kuogopwa kama Ukoma!

    Ahsante sana Mhe. Dr.Harriosn Mwakyembe kwa kurejesha safari za treni Reli ya Kati!

    Nani kama Mwakyembe?

    ReplyDelete
  5. Kwa maisha ya vijiji hivi, Tereni ikipita ndio kama hukupata Ukakope!

    Ama sivyo hadi treni ijayo!!!

    ReplyDelete
  6. ahhh Ankali!

    Picha za nmna hii zitatukwamisha jitihada za kuwashauri Madiaspora ndugu zetu Majuu kurudi nyumbani!

    Kama ujuavyo ndugu zetu ni waoga sana wa shida na changamoto za kimaisha.

    Hivi Licha ya hao wa Majuu sisi wa hapa Bongo Darisalama si ni vigumu mtu kuamini kama unaweza kumudu maisha kwa mauzo ya majogoo matatu (3) tu mkononi?, tena Treni baada ya treni siku 3 au wiki mara moja?

    ReplyDelete
  7. hehehehehe inanikubmusha Mbali sana usafiri wa Treni!

    Jamaa mmoja alikwenda Kijijini ambako anashukia Kijiji cha umbali fulani ndio afike Kijijini kwao.

    Alipofika Kijijini alikaa kwa siku 5, na mara muda wa kuondoka ulifika akaaga akaondoka kwenda Kijiji chenye Usafiri wa Treni ambako ndio hupita.

    Kawaida Treni hapo hupita saa 3 za asubuhi kila baada ya siku 2.

    Siku ya 1, alilala Kilabuni baada ya kunywa mpaka masaa mengi alipozinduka ilikuwa ni saa 4 asubihi na Treni ilikwisha pita.

    Akakaa siku mbili kusubiri, huku siku hizo akizitumia na wenzake Kilabuni kwa kunywa, ilipofika siku Treni inakuja akaenda kumuaga rafiki walikuwa wote wanakunywa pamoja kurudi Stesheni akakuta ndio Treni inaondoka inapiga honi!

    Jamaa aka ghairi safari kwa mara ya pili, huku akiwa anatumia akaanza kukopa Kilabuni akinywa na wenzake,,,mara Mama Mpikaji Pombe akataka fedha zake jamaa akawa hana ameishiwa ikabidi apewe jembe akalime, na Ikawa ndio amelizima akawa mkazi wa Kijijini hadi leo!

    Kisa hiki kinamtaja mtu mmoja alikuwa anaitwa Diha!

    ReplyDelete
  8. Treni hiyo kumbukumbu nzuri ya utawala wa Kijerumani.Waingereza hovyo kabisa

    Nje ya mada-Huwa nasikia wazee vijijini wanasema tulitawaliwa na Wadachi-Waholanzi?(wakimaanisha Deutsche nadhani, siyo Dutch).Kuna uhusiano wowote kati ya DUTCH na DEUTSCHE?.Nilimwuliza rafiki yangu msomi tu Royal Dutch Airline ni shirika la ndege la nchi gani akanijibu UJERUMANI(kwa sababu ya neno Dutch(Wadachi),nikamwuliza je Deutsche Welle Radio?akapata akasema ni ya Ujerumani.

    David V

    ReplyDelete
  9. Mjomba Michu,

    Hapa andika Wanakijiji wapo kwenye Sherehe za kukamilisha Msimu wa Mavuno na sio ndio wapo kazini kutafuta Maisha.

    Hii itawatisha wa Majuu kurudi nyumbani kuona watu Bongo wanaendesha maisha kwa mauzo ya nyungo na majamvi ,majogoo na Makapu!

    Sasa je ina maana hata Polisi walitegemea Mshahara pekee mwezi hadi mwezi (bila Rushwa) kwa miezi yote iliyosimama usafiri wa reli ?

    ReplyDelete
  10. Isipokuwa pamoja na ugumu wa maisha watu wanagali ni majasiri sana,

    Kwa hali hiyo ya mauzo na uchumi wa hali jojo hapo Kijijini utakuta watu akitoka hapo:

    -Anaanzia kwenye Banda la Gongo!

    -Anaanzia kwenye matapu tapu na makalapusi ya Ulevi!

    -Anaanzia nyumba ndogo!

    -Ukimkuta Kilabuni anaagiza utadhani ni Bilionea anajiamini!

    -Anakuwa jasiri hata kama Treni lilipita na hakuuza kitu!

    Iwe treni ilipita akauza au hajauza,

    Licha ya kuwa Uwezo wenyewe Kiuchumi ni wa mauzo ya majogoo matatu (3) tu mkononi!

    Majukumu yanaisha maishani?

    ReplyDelete
  11. TSPCA:

    Haki za Wanyama mpooo!

    Wewe Alhaji wa picha ya pili na ya tatu kutoka chini, hivi Ustaaadhi kama ingekuwa ni wewe ungekubali kubebwa kichwa chini miguu juu?

    Kwa nini usitafute Boksi au Tenga kuku hao ukawaweka?

    Hata kama wanakwenda kuchinjwa huko kwa huyo utakaye muuzia,

    Zingatia ya kuwa hao kuku ni viumbe kama wewe, hivyo wanastahili pia haki!

    ReplyDelete
  12. Haya maisha kila mtu na ya kwake!

    Licha ya Uchumi kuwa wa kuyumba hapo Kijijini, wakati mzunguko wa kifedha ni Treni hadi Treni ikipita kila baada ya siku kadhaa labda baada ya siku 2 au 3 kwa wiki, unakuta mtu anamaliza bidhaa Treni inapiga honi (POOOOOOOOOOOOOOLIIIIILOOOOOO)!!!

    (FYUUUUUUUU, PSUUUUUUUUUU, FYAFYA FYA ,) !!!,,,mipira ya breki za Upepo inafunguka.

    (KWATA, KWATA,KWATA,KWATA)!!!,,,magurudumu yanazunguka.

    Treni inaondoka!

    Bingwa muuzaji bidhaa Stesheni huyooo, anakusanya virago na Gunia lake alilotandika chini kuuzia, anaanzia kwenye Kilabu cha Kangara anapiga kiberiti fedha yote aliyoipata siku hiyo!, Kipato kingine ni hadi Treni ingine ikija!

    ReplyDelete
  13. Hapo ni kuwa Uchumi unakuwa kaburini siku ambazo treni haipiti, siku ikipita ndio uchumi unafufuka na kuwa hai!

    Ukimdai mtu, atatoa sababu ohhh wewe unajua treni haijapita, ikipita tu nitakulipa!

    Mfano isipotokea labda ratiba imesimama hakuna jinsi hapo Kijijini mwanawane utafikia lengo kwa kazi hizi zikiwa na changamoto zake:

    1.Utakata mkaa, UKIKABILIANA NA MAAFISA WA MALI ASILI kuhusu vibali!

    2.Utapakua asali ya miamba Msituni, UKIKABILIANA NA MAAFISA WA MALI ASILI kwa suala la vibali na Misitu ya Hifadhi!,

    3.Uwindaji Porini, UTAKABILIANA NA MAAFISA WA WANYAMA PORI kwa vibali na Vitalu vya Uwindaji!

    4.Utauza Gongo Kijijini ,UTAKABILIANA NA MGAMBO WA KATA (sio Polisi) kwa vile Kituo cha Polisi kipo Stesheni ya tatu kutoka hapo!

    5.Utakuwa Pusha wa Ganja Kijijini, UTAKABILIANA NA POLISI JAMII WA KIJIJI NA MGAMBO WA KATA!, ahhhh ukikwama hapo hakuna pa kukimbilia!

    ReplyDelete
  14. Mhe.Dr.Harrisson Mwakyembe:

    Si Dikteta wala si Masiya, bali ni Mtendanji Mkuu mwenye Muono!
    -----------------------------------

    ''RWANDA INC.''

    He neither a Dictator nor a Messiah, but he is a CEO with a vision!

    Hayo ni maneno ya Utangulizi wa Kitabu kinachomzungumzia Raisi Paul Kagame wa Rwanda kwa utendaji wake ambacho kimeadikwa na wanamama wawili wa Kimarekani.
    -----------------------------------

    Maneno hayo na Utangulizi yanastahili sisi Watanzania, hasa walio katika mstari wa reli tuupambe wasifu wa Mhe. Dr.Mwakyembe kwa jinsi alivyoweza kurudisha matumaini ya maisha kupitia Usafiri wa reli!

    ReplyDelete
  15. Hapo mtu akikopa kwako?,

    Ohhh umeliwa atakwambia hadi treni iwasili (HATA KAMA IMESIMAMISHA SAFARI ZAKE NA ITAANZA BAADA YA MIEZI 6) ndio ataweza kukulipa!

    ReplyDelete
  16. Kwa kurudisha matumaini ya maisha?

    Wakazi wa Ukanda wa Reli kwakweli watamwona Mhe.Dr. Mwakyembe kama Nabii!

    ReplyDelete
  17. Uchumi wa hapo unakwenda kama homa za vipindi, treni ikiwasili uchumi upo waa kila mtu ana jeuri na tajiri!

    Treni isipokuja, ohhh usimlaumu mtu hasa kama unamdai ni vile inafahamika moja kwa moja ya kuwa uchumi upo likizo.!

    Hata kama Utamfikisha kwa malalamiko Ofisi ya Mtendaji, ni wazi utakuwa umeshindwa kwa hoja , kwa kuwa hata Mtendaji wa Kijiji atamtetea jamaa (Mdaiwa) ya kuwa hawezi kukulipa kwa kuwa treni haijawasili!

    ReplyDelete
  18. La jamani tujitahidi angalau tutoke kwenye Mstari huu wa Umasikini wa CHINI YA DOLA MOJA YA MAREKANI kimaisha.

    Angalau tujivute kwenye masuala haya ya Gesi ,Mafuta na Madini ili iwe Kombolela kwa wenzetu kwamba maisha ni kama mchezo wa Kombolela Butua uwaokoe wenzako, ili na sisi tuondokane na huu Uchumi wa kuti kavu wa kutegemea mauzo ya majogoo na mikeka Stesheni za treni!

    ReplyDelete
  19. Treni isipowasili kwa siku kadhaa,,,uwezekano uliobaki ni kuchukua pipa ama mtungi na kuchemsha pombe ya kienyeji ya Kangara!

    Ofisi ya Kikazi inahamia Kilabuni kutoka Stesheni ya treni.

    ReplyDelete
  20. Kuku wanabebwa Kichwa Chini!!!! Huu ni ukiukwaji wa haki za wanyama.

    ReplyDelete
  21. Ohhh naenda Kijijini nachukua nauli peke yake itanitosha,,,mara pyeee Mwakyembe amesimamisha kwa muda safari za treni wakati wewe Kijijini akiba imekatika.

    Hapo lililobaki ni kuingia msituni na kuchimba miti shamba na kugeuka Maganga wa Kienyeji Kijijini hadi treni ianze safari upya!

    ReplyDelete
  22. Sasa ndugu yangu UNANIDAI VIPI WAKATI TRENI HAIPITI SIKU HIZI, hebu nieleze nitakulipa vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...