Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Job Lusinde akitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,alhamisi januari 24, 2013 ambapo alikutana na wajumbe wa Tume hiyo kutoa maoni na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya. Anayemwongoza ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na wa kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani.
Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Ibrahim Kaduma akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Tume hiyo, alhamisi januari 24, 2013 ambapo alitoa maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiagana na Waziri mstaafu na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Job Lusinde mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Tume hiyo, ambapo alitoa maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Ibarahim Kaduma akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba mara mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Tume hiyo, ambapo alitoa maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. . Mwingine ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dkt. Salim Ahmed Salim. (PICHA NA TUME YA KATIBA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. haya maoni yanakusanyiwa hapo Dar tuu mbona hawa jamaa hawazunguki nchi nzima?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...