Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar akiwa na Mzee wa changamoto wetu, Mubelwa Bandio, katika mahojiano yaliofanyika Siku ya Jumanne January 8, 2013 ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC Nchini Marekani. (Picha na swahilivilla.blog)
Hii ni sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano kati ya JAMII PRODUCTION na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico (anayemaliza muda wake) Mhe. Mwanaidi S. Maajar
Katika sehemu ya kwanza anaeleza
1: Historia ya maisha yake (kwa ufupi)
2: Ilikuwaje akaingia katika fani ya sheria? Na ni nini alipanga kufanya kabla ya kuamua kuwa mwanasheria?
3: Ni vipi alipokea ombi la kuwa Balozi?
4: Ni changamoto zipi anazokutana nazo kwenye kazi yake ya ubalozi?
5: Ni vipi anabadili mawazo ya waMarekani wanaoiona Tanzania kama nchi isiyopiga hatua?
6: Anawashirikisha vipi viongozi wa Tanzania katika maendeleo anayoyaona Marekani?
7: Ipi nafasi ya mwanamke katika uongozi?
8: Anazungumzia vipi suala la viti maalum kwa wanawake?
9: Je! Tanzania ipo tayari kuwa na Rais mwanamke? Na Je! Tanzania ina wanawake ambao wanaweza kuwa rais wa nchi?
Na mengine mengi.
KARIBU UUNGANE NASI
mama yangu alisoma na huyu balozi shule ya weru weru na anasema akikuwa hard working sana kama mwanafunzi pale. sasa mheshimiwa ukirudi tanzania jitahidi ukipata muda ufanye mihadhara kwenye shule za wasichana kuwapa moyo. au kama ikiwezekana uandike kitabu cha historia ya maisha yako kuelezea jitihada zako kama mwanamke. wengi wa kina dada wa sasa wakiwa na haiba za kuvutia wanachofikiria ni kuolewa na mtu tajiri na kustarehe!! nadhani hawa kina dada wa sasa wanakosa motivation....
ReplyDeletenimefurahi sana kumsikia huyu mama maana ananipa furaha ya kua mtanzania.ukirudi uongee na magazeti yawe yanaandika vitu vitofautiane angalau kidogo.watafute habari huko vijijini.
ReplyDeletemama ni role model.bado tunakukumbuka uingereza ukituunganisha.hope mh atatuletea mama tena hapo marekani.endelea na moyo wako mkarimu mama.
ReplyDeletesalama of Mkasi TV should learn from this interview on how the whole thing is conducted. Look how well structured is this interview. Salama and John you have a lot to learn!!!!
ReplyDelete