USIKU wa kuadhimisha kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2013 ulishuhudia burudani ya kukata na shoka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala, ambapo wasanii kadhaa wa muziki wa kizazi kipya walitoa burudani ya kufa mtu. Wasanii ambao waliwafanya mashabiki wasitulie katika viti vyao ni wakongwe Profesa J, Inspekta, Juma Nature, pamoja na wasanii wanaokuja juu katika fani hiyo ambao ni Linex na Stamina, huku bendi ya African Star ‘Twanga Pepeta’ wakiwapindisha migongo mashabiki.Pichani ni Juma Nature akiwapagawisha mashabiki.
Mkongwe Profesa J akiwapelekesha puta mashabiki.
Linex akiwapagawisha mashabiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...