Mdau Shaban Leo wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi akifurahia baada ya kufunga pingu za maisha na mai waifu wake Pendo Kuboga wa manispaa ya Lindi pia. Ndoa ilifungwa katika kanisa la Waadventista wasabato Mtaa wa Lindi na Tafrija ya kuwapongeza ilifanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Mt Andrea Kaggwa.Picha na Abdulaziz Video.
Maharusi na Wapambe wao wakiwa kwenye nyuso za furaha.
Maharusi wakipewa Baraka ya Ndoa toka kwa Mchungaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongereni Wanandoa wapya. Mibaraka ya Mungu izidi kumiminika kwenu. Amen

    ReplyDelete
  2. Enheee ninyi Wapambe wa Maharusi Picha ya 2 juu kushoto msije mkalianzisha kwa kuwa ninyi mpo kama sample lakini mmekaa 'zero distance' kiasi kwamba yasije yakatokea Mapindizi halafu wakatokea wa kulalamika!

    Mara nyingi Wapambe wa Maharusi hutokea wakazimikiana na kitu kikaeleweka, pia wanaocheza Sinema wakiwa kama mtu na mpenziwe ama mtu na mkewe hutokea wakachukuana kikweli!

    Kwa mtaji huu manafikiri baada ya jukumu la Upambe kwenye Harusi haiwezi tokea patashika?

    ReplyDelete
  3. Ohoooo !

    Wapambezzzzz picha ya pili juu,

    1.Mbona mmekaa mkao wa kula?
    2.Mbona mmekaa mkao wa 'Shemeji shemeji huku unazima taa'?

    Je, kama mna wenzenu kila mmoja wenu hapo watawaelewa vipi?

    ReplyDelete
  4. wapambe ni mtu na mkewe acheni jazba

    ReplyDelete
  5. Any wa pili mara nyingi ndoa za kikristu wapambe lazima wawe wanandoa.

    ReplyDelete
  6. Hiyo picha ya kwanza ya maharusi na hasa huo ufukwe ambao wamekaa ni tambarare ya ufukwe ambao unakuleta mpaka upande wa chuo cha maafisa tatibu lindi nilipopata diploma yangu na ndipo safari yangu ya kuusaka uhadhiri ilipoanzia, nashukuru mungu sasa nipo canada kama mwanasayansi dakitari.Na upande wa pili wa maji yaani kule kulikokua na ukijani kulikua kuna simba wengi na chui nakumbuka kila siku tulikua tunahudumia majeruhi wa chui au simba. Asante sana kwa picha hii yenye ukumbusho tosha.

    ReplyDelete
  7. Wabongo kwa ngebe tu, hakuna wakufananisha.

    ReplyDelete
  8. siwafahamu lakini hongereni sana maharusi.
    harusi simple isiyo na makuu
    mungu awabariki katika ndoa.
    Mdau Alabama USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...