Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akizungumza na wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni ya Simu ya TTCL na migogoro iliyopo kwenye Kampuni ya hiyo. Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said (kushoto) akitoa muongozo kwa wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni hiyo ya TTCL na migogoro iliyopo,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Karim Bablia akitoa kero mbali mbali alizokumbana nazo kwenye kampuni hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni hiyo na migogoro iliyopo,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa TTCL,Shaban Mrisho wakisikiliza kwa makini kero mbali mbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam,leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL jijini Dar es Salaam na Wafanyakazi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakifatilia Mkutano huo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akiendelea kuongea na Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam leo.

KWA PICHA ZAIDI TEMBELEA 
http://othmanmichuzi.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Management yote ingefumuliwa na kuundwa nyingine maana migogoro iliyopo ndani ya TTCL inatokana na management mbovu

    ReplyDelete
  2. Ita saidia sana Muchuzi kama kuna speech ya Young Mhe. Makamba.Asante

    ReplyDelete
  3. what about wafanyakazi ndiyo bomu. watimuliwe wao,

    ReplyDelete
  4. I agree the ttcl should be dissolved and give a fresh start....Lakini we want January to be the next President of Tanzania....January Oyeeeeee!

    ReplyDelete

  5. hiyo ndiyo tofauti kubwa ya private sector na govt.sector. kampuni za watu binafsi za simu zinafanya vizuri sana kwa kuwahudumia wananchi kwahiyo hakuna haja tena ya watanzania kutumia kodi yao kuendesha makampuni yanayoleta hasara wakati wanaweza kupata huduma safi kutoka kwa kampuni binafsi. wakati wa kulea uozo kwa sababu eti ni shirika la umma umeisha. wananchi watapiga kura kwa kutumia wallet zao kuamua nani anafaa na nani hafai hiyo ndio free market.

    ReplyDelete
  6. TTCL WAMEZIDI KWA USUMBUFU HATA KAMA UTAPIGA SIMU KUOMBA MSAADA WATAKUWEKA KWENYE LINE THEN WATAKATA SIMU BILA MAJIBU. UKIPIGA TENA UTAWASIKIA WANAJIBIZANA WAKUPE JIBU GANI NONSENSE KABISA.

    ReplyDelete
  7. Msiwaonee bure TTCL,samaki mmoja akioza,basi wote wameoza?No,thats gross generalisation!Toeni Hoja hapa,nini kifanyike ili kuimarisha huduma za TTCL,badala ya kurusha madongo tu na kuishia kulaumu.Serikali iwe serious,ziuzwe Hisa za TTCL kwa Watanzania,say,a certain %,say 40% to 55%!,Hisa zilizobaki,ziuzwe kwa Serious Private Investors,both foreign and local!Serikali iteue Professional Management Firm moja,ifanye Feasibility Study(around six months deadline),itoe mapendekezo nini kifanyike,"lakini sio ku i dump TTCL,kwa bei ya Korosho"kama ilivyo fanyika kwa mashirika mengine ya Umma!Mazuri yazingatiwe,Mabaya yatupiliwe mbali,Tuanzie Hapo,badala ya kuendeleza "Longolongo zisizo na msingi"!Wafanyakazi wenyewe wa TTCL wapewe mgao fulani wa hizo hisa zitakazo uzwa!Nina hakika kwa taratibu hizo TTCL itakuwa na nguvu na kufanya maajabu!(silent voice)!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...