Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, Mkurugenzi Tiba Dr. Salhia Ali Muhsin na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wakifurahia na kuangalia vifaa mbali mbali walivyovitoa kwa ajili ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Wilaya ya Kaskazini “A”.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mwanamwema Sehni akikabidhi Viti vya Wagonjwa kwa Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Dr. Salhia Ali Muhsin hapo katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akizungumza na wanachama wa Nungwi Saccos hapo katika Tawi la CCM Nungwi.Kushoto kwake ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi ,na Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Uwt Zanzibar Bibi Salama Aboud Talib.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akithibitisha rasmi kutekeleza ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete ya kukabidhi mchango wa shilingi 2,000,000/- Ushirika wa Nungwi Saccos.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akikabidhi mchango wa shilingi 2,000,000/- kwa kikundi cha Nungwi Saccos kutekeleza ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Slma Kikwete aliyoitoa mwezi Mei mwaka 2010.
Akina mama wa Ushirika wa Nungwi Saccos wakishangiria mchango wa shilingi milioni 2,000,000/- zilizotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni ambazo ziliahidiwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete wakati akiizindua Nungwi Saccos Mwaka 2010.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...