Habari Kiongozi

Nimeona nikurushie taswira hizo za barabara ya Namtumbo - Tunduru ambayo Mkandalasi wa Kampuni ya Progressive amefungishwa virago baada ya kushindwa kuitengeneza. 

Hivi sasa hali ni mbaya, magari ya abiria na mizigo yamekwama na mengine yameharibika kabisa na kuna tishio kubwa kwamba barabara itajifunga sio muda mrefu kwa sababu mvua hasa bado hazijaanza.

Mkandalasi aliyekua akitengeneza alipewa ushindi wa vipande vitatu avitengeneze kwa kiwango cha lami na matokeo yake kashindwa, hadi anatangazwa rasmi kuondolewa Januari 08, 2013 ilikua tayari miaka miwili imepita tangu apewe kazi hiyo iliyopaswa kufanywa mwa muda wa miezi 28 na kazi aliyofanya haifiki hata asilimia 5.

So kutimuliwa hajaonewa.

Mdau RUVUMA
Hapa ni Baadhi ya abiria wa moja ya mabasi yanayotumia barabara hiyo wakiwa wamekaa chini ya kivuli cha mti wakisubiri basi lao lililokwama,ili litoke na waendelee na safari.
Hapa jamaa wamehangaina na basi lao mpaka wamechoka,hivyo wakaamua tu kuweka mapozi ili wajipatie picha za ukumbusho.
hivi ndivyo mambo yalivyo kwenye barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Naipa pongezi serikali kwa juhudi inazofanya ktk kuboresha miundo mbinu,ila huyu mkandarasi nimeshangaa kusikia bado alikuwepo na zabuni alishinda vipi,maana miaka miwili ilopita nilibahatika kupita njia hiyo na nikaona gari moja tu na mashine moja tena vikitengenezwa sio vikifanya kazi.ile ni barabara muhimu sana kama ikikamilishwa.

    ReplyDelete
  2. Duh! Poleni....
    Je kufurushwa tu inatosha! Ama ndiyo suluhisho!?
    Je Uwezo, weledi na uadilifu wa tunayetarajia kumpa kazi/kandarasi tuupimie wapi na lini?! Ifike mahali tunaowapa kazi tuwapongeze na si kuwafurusha!!

    ReplyDelete
  3. Hii ndo habari imekamilika kwa picha kuelezea hali halisi ya mradi huo wa ujenzi wa barabara.

    Heko wadau wa blogu ya jamii kwa kutoa habari kama ilivyo pamoja na picha kuelezea kama mradi umefanikiwa au la.

    ReplyDelete
  4. Du poleni sana wakazi wa kusini,ipo siku mtaiona nafuu kafurahia matunda ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...