Mwenyekiti wa Mkutano Kujajidili Changamoto za Muungano,Mh. Mohamed Aboud Mohamed ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akijadiliana jambo na Mwenyekiti Mwenza,Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano wakati kwa mkutano huo.
Baadhi ya Mawaziri wakiwa katika mkutano wa kujadili Changamoto za Muungano mjini Zanzibar leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Fedha,Uchumi na Maendeleo Zanzibar,Mh. Omary Yusuph Mzee (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. William Mgimwa wakati wa mkutano huo.Picha na Ali Meja, Habari na Evelyn Mkokoi wa OMR.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar mh. Mohamed
Aboud Mohamed, ameongoza kikao cha mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichojadili masuala ya muungano huko Zanzibar
leo.
Mambo mbali
mbali yamejadiliwa katika kikao hicho, ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha
kumbukumbu za kikao cha Mawaziri kilichopita kilichofanyika mjini Dar es Salaam
mwezi march mwka 2011, kupitia kumbu kumbu za kikao cha kamati ya pamoja ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Seriklai ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mh. Aboud kama
mwenyikiti wa kikao hicho cha mawaziri pia ameongoza mawaziri hao katika
kupitia rasimu ya mwongozo wa ushiriki wa serilaki ya mapinduzi Zanziar katika
masuala ya kimatifa katika hatua za awali.
Pamoja na hayo
mambo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na,kupokea mapendekezo kuhusu uratibu wa
muda wa mgao wa ajira kwa taasisi za muungano kwa serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kupitia taarifa ya
utekelezaji wa masuala ya muungano.
Aidha kikao
hicho pia kimeweza kupitia hati za makubaliano ya hoja zilizopatiwa ufumbuzi,
na agenda za kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali
ya mapinduzi ya Zanzibar .
Mwenyikiti Mh.
Aboud ameongoza kikao hiki cha mawaziri kwa kushirikiana na mwenyekiti
mwenza ambae ni waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais muungano Mhe. Samia Hassan Suluhu ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya kikao cha kamati ya pamoja kati ya serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
na serikali ya mapinduzi Zanzibar kitakachofanyika kesho mjini zanzibar chini
ya uwenyekiti wa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Dkt Gharib Mohamed Bilal.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...