Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akifungua kituo cha kompyuta cha kanisa Anglikani Parishi ya Magugu (Mkoa wa Manyara) Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro jana.
Mwanafunzi Idrisa Hassan akimuonesha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, viongozi na waumini wa kanisa Anglikani Magugu namna ya kutumia kompyuta wakati wa ufunguzi wa kituo cha kutolea elimu ya Komputa cha kanisa Anglikani Magugu, hafla ya ufunguzi ilifanyika kanisani hapo mapema jana.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanajifunza elimu ya komputa kwenye kituo cha kutolea elimu ya komputa cha kanisa Anglikana Magugu kilichofunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi mapema jana .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na Baadhi ya wanafunzi na Waumini wa Kanisa hiyo mara baada ya ufunguzi kituo cha kompyuta cha kanisa Anglikani Parishi ya Magugu (Mkoa wa Manyara) Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro jana.
Katibu wa kanisa Anglikani parishi ya Magugu Bw.Dismas Charles akisoma taarifa fupi ya kituo cha kompyuta kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimb, uongozi wa kanisa na waumini wakati wa hafla ya kukifungua kituo hiko.
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA DR R. NCHIMBI KWA KUJISHUGHULISHA SANA NA MAMBO YA KIJAMII. UMEKUWA NI MTU WA KUJISHUSHA NA KUWASIKILIZA WATU WA NAMNA TOFAUTI BILA KUJALI UWEZO WAO. WEWE NI MFANO WA KUIGWA.

    ReplyDelete
  2. Hongera Dr. Nchimbi, watu wachache sana wenye moyo kama wako nchi hii. MUNGU akubariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...