MTOTO SAMWEL MLOPE

Unaweza kujiuliza ni nini ambacho kimetokeza katika mgongo wa mtoto huyu?.Mtoto Samwel Mlope mwenye umri wa miaka kumi na moja(11) ambaye ni mkazi wa Mahenge ndani ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Mtoto huyu alianza kuumwa mwaka 2001 ambapo alianza kusumbuliwa na tatizo la moyo kuwa na tundu.

Kwa mara ya kwanza kabisa alipoanza kusumbuliwa na tatizo hili mama yake mzazi ambaye ni Bi. Amina Ally alimpeleka katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na baadae akaambiwa ampeleke mtoto huyo katika hospital ya Taifa Muhimbili na baada ya kufika muhumbili ndipo alipoambiwa kuwa mtoto Samwel anasumbuliwa na tatizo la kuwa na tundu kwenye moyo wake.
Afya ya mtoto Samwel wala hairidhishi kabisa,hali iliyompelekea kushidwa kabisa hata kupata masomo.
Na huyu ndiye mama mzazi wa mtoto Samwel Mrope,Bi. Amina Ally ambaye anajishughulisha na kazi za ndani ili aweze kujipatia pesa kwa ajili ya kujikimu kimaisha yeye pamoja na mwanae samwel. Alisema kuwa "baba wa mtoto Samwel aliondoka muda mrefu sana uliopita kuelekea machimbo kwa ajili ya kutafuta na mpaka hii leo hajarudi na hawafahamu yupo wapi.

Bi. Amina alisema kuwa "ninawaomba watanzania wote kwa ujumla waweze kunisaidia ili mwanangu Samwel aweze kupelekwa nchini India na kupata matibabu kwani mwanangu anapata shida sana"na hatimaye aliweza kuzitoa namba zake za simu kwa watu ambao watajitokeza kutoa msaada kwa mtoto Samwel ambazo ni 0752 732290.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nadhani kabla ya kufikiria india pengine ingekua vizuri tukaanza kufikiria taasisi yetu ya kizalendo ya magonjwa ya moyo THI(Tanzania Heart Institute)wakajaribu kumuona mgonjwa iwapo wataridhika mgonjwa apelekwe nje basi lifanyike hilo na si tu kuanza na india.Huu ndio mchango wangu wa mawazo.

    ReplyDelete
  2. michuzi hebu muunganishe huyo mama na chama cha Rotary International Dar Chapter,Lions Club,hata wizara ya afya;ili mtoto huyo naye anufaike na misaada inayotolewa na taasisi hizo!msipoteze muda na "mabakuli",ugonjwa wa moyo unahitaji tiba ya haraka sana!Mungu amzidishie uhai na apate msaada huo mapema iwezekanavyo!Kwake Mungu hakuna litakalo shindikana!viongozi wa taasisi za kidini,wenye uwezo au marafiki huko nje,wajaribu kufanya kila liwezekanalo!Leo,mtoto huyu,kesho wewe na mimi!Atakaye kuzika humjui!Shime,tusaidiane mawazo ya hali na mali!amina!

    ReplyDelete
  3. Tafadhali mpeleke Regency Hospital naye ataelekezwa na kupatiwa msaada wa kwenda India. Labda cha kufanya mama achukue documents zote za mtoto na kwenda naye. Nitarudi nchini next week on Wednesday, nitakutumia fedha kwenye tigo pesa ile uweze kuja na mtoto Dar es salaam. Bahati mbaya mimi ni mtu wa safari nyingi. Je ana ndugu hapo Dar es salaam wa kuwa anamsindikiza Regency na wa kufikia kwake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...