Kamera ya Globu ya Jamii,imemnasa Binti huyu ambaye jina lake halikufahamika mara moja katika Maeneo ya Kamata Kariakoo akijitafutia riziki yake kwa kujishughulisha na usafishaji wa Vioo vya Magari ya watu yanayokuwa yamesimama kwenye Mataa ya Kuongozea Magari.Kwa kawaida imezoeleka kuonekana vijana wa kiume ndio wanaoonekana kujishughulisha na kazi hii sehemu kubwa ya jiji la Dar na si wa kike kama alivyoonekana huyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Ahsante uncle kwa kututumia picha ya binti huyu katika blog. Lakini kwa upande wangu picha hii imenipa hisia mbili tofauti. Hisia ya mwanzo nimeshukuru kuona kwamba kijana huyu wa kike ameamua kuchukua njia ndefu na ngumu na siyo ya mkato kama vile kuwa kichangu katika kujitafutia maisha na kujipatia ridhiki mtego ambao vijana wengi wa kike wenye myumbo kimaisha wamekuwa wakiangukia.

    lakini upande mwingine nimejiuliza maswali mengi na kupata fadhaa kuwa kijana wa kike wa umri huu alionao amekumbwa na matatizo gani kifamilia mpaka kujikuta hapo alipo na akifanya kazi anayoifanya. kwani kwa makisio yangu huu ni umri wa kuwa shuleni au chuoni kujipatia elimu ya kumjenga kimaisha. wadau simlaumu huyu binti ila muhimu ninachotaka changia ni kuwa kwa nini binti huyu asitafutwe akaulizwa mashaka yanayomsibu na ikiwa yu tayari kurudi shuleni sisi wadau wa blog hii tukaanzisha donation tukamrudisha binti shuleni na kumpa nafasi ya kuishi maisha bora? hili linawezekana na tunaweza kupitia michuzi blog tukaweka historia na kuboresha utamaduni wa kusaidia wenye matatizo ndugu watanzania. huyu asiwe ni burudani tu ya kumsoma na kubaki kumsikitikia au kumsifia kwa ujasiri, ukweli analofanya si sahihi kwa umri wake ni ugumu wa maisha tu, na hili twaweza kulirekebisha kwa msaada mdogo wa kumfikisha kidato cha nne kwa kuanzia, kwa gharama ndogo tu. uncle michuzi ikiwa huyu binti anachotaka ni elimu na wazazi hawana uwezo wa kufanya hilo mimi nashauri ianzishwe harambee kupitia blog hii tumsaidie huyu binti. AHSANTE

    BY Mitkasi, UK

    ReplyDelete
  2. Bongo Tambarale!

    Wala huhitaji kujidhalilisha kwa Uchangu, kuiba wala kutumia nguvu unahitaji kutumia bidii na akili.

    Bibie anapata zake za Dona na Mbaazi!

    ReplyDelete
  3. Mdau Mitkasi wa UK Anony wa Sat Jan 12, 04:13:00 AM 2013

    Unaonekana kuwa na moyo na Harambee kwa wenye shida.

    Licha ya huyu Binti mwosha vioo vya magari barabarani pana Harambee ingine iliyokuwa inajadiliwa humu karibu wiki hii nzima ya Malezi ya Mapacha watatu wa ndugu yetu Edwin Rwechungura wasiliana na Michu kwa yote mawili huyu Binti na Watoto mapacha wa 3.

    Pamoja tutajenga!

    ReplyDelete
  4. Hao vijana ni TIMING Bombs nasi tunaangalia bila kuchukua hatua. Hivi umeshaona vitendo wanavyofanya katika maeneo hayo?

    ReplyDelete
  5. Balozi mimi naungana na mdau hapo juu. Tuanze na huyu dada kupitia globu hii.mwaka 2013 uwe wa mabadiliko.

    ReplyDelete
  6. @mitkasi, nakubaliana na wewe! Wallah inatia huruma maisha yetu yalivyo ktk hali mbaya, huyu dada ameamua kufanya kazi hii ili apate rizki yake ya halali.
    ingekua wengine wangejiingiza ktk mambo mengine, i hope viongozi wetu wanaona picha hizi.

    Asante uncle

    ReplyDelete
  7. SITASHANGAA KUSIKIA HUYU BINTI ANAFANYISHWA KAZI ZA VIBARUA NA MTU/WATU WALIOMTOA KWAO KWA AHADI ZA MAISHA MAZURI MJINI. HII IPO SANA WADAU, CHUNGUZENI

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza unanishangaza kidogo. Kwa hiyo ndiyo kusema unaona ni sawa kwa watoto wa kiume wenye umri kama wake wafanye hii kazi badala ya kwenda shuleni na si wasichana? Unamaanisha watoto wakiume wa umri wake hawahiitaji hiyo harambee? Kama ni harambee iwe kwa wote na siyo kwake tu kisa ni msichana?

    ReplyDelete
  9. wewe huoni kama huyu ni street chilreen amekua sasa anaanza kujifanya kuosha vioo ili asaidiwe kwa namna hiyo? logwa umchukue akafanye kazi za ndani kwako uone.. utajuta kuzaliwa.hayo ndio maisha yake aliyojichagulia bwn tusiumize vichwa tuna mengi ya kufanya.

    ReplyDelete
  10. Bongo akili kichwani!

    Bongo ugali kwa kichwa cha kambare!

    Bongo nusu mkate!

    Fanya uwezalo ili mradi usiyakanyage ukavunja Sheria za Kiraia na za Jinai (achilia mbali sheria za Kibiashara hizo weka kibindoni, wakija Mgambo wa Manispaa wakatie dona na mbaazi endelea na kazi yako).

    Bibe ameona Uchangu sio njia sahihi kufikia malengo ya kimaisha, huyu ni Jasiri sana anafaa Kimaisha...jembe la Kike.

    Ukimweka mkononi huyo ni lazima utatoka Kimaisha!

    Masela mliopo Majuu na wa hapa Bongo Tambarale mmemuona Mpiganaji bibie?

    ReplyDelete
  11. Mimi Maganga huku Sweden napata tabu ya bureee sina msaidizi mimi ni Carwash hapa kwa miaka 15 sasa.

    Nitachukua Pasipoti yangu ya Kisweden nikamchukue msichana MCHUMBA jasiri nije naye najua nitapiga mabao.

    Huku Sweden ataosha magari kwa EURO 15 (Tsh. 29,250/= kwa kila gari) badala ya Tsh. 1,000 kila gari Bongo!

    ReplyDelete
  12. ANON WA KWANZA, UMESEMA KWELI KABISA. NAKUUNGA MKONO MIA KWA MIA.

    UWEZEKANO MKUBWA SANA ATAKUWA NI MTOTO WA OMBAOMBA.
    WATOTO WA OMBAOMBA NI ASILIMIA KUBWA SANA YA WATOTO WA MITAANI. KILIANZISHWA KITENGO NA USTAWI WA JAMII WAKAWA WANAITWA KULEANA. MAZINGIRA HAYAKUWA MAZURI NA HAIKUWA RAHISI KUTEKELEZA LENGO.
    WAKO WENGI SANA, NA WANAENDELEA KUZALIWA.

    USTAWI WA JAMII INAELEKEA UMESHINDWA, UNATUPIA MPIRA RAIA "KUSAIDIANA".

    RAIA TUTASAIDIANA KWENYE ISOLATED CASES TU. WATOTO WA MITAANI WAKO WENGI SANA KUSAIDIWA KI HARAMBEE HARAMBEE. NI JANGA NA "EYESORE" YA TAIFA.

    TATIZO HAPA NI SYSTEM NZIMA IME COLLAPSE

    ReplyDelete
  13. Michuzi Chukrani nyingi kwa kutuwekea tukioa kama hilo nafikiri wengi wetu watakao soma na kuiona hii habari itawagusa kiasi fulani hata kama wanatokana na familia zenye uwezo ,ukizingatia zaidi hii habari imegusa kwa msichana inakupelekea mtu kuwaza mzazi wako wa kike na mihangaiko ya maisha na ugumu katika nchi kama hii ,swali langu hapa Mchukuwa picha wako au kama ni wewe mwenyewe ulifanya angalau kumdadisi ukajuwa nini kinachomsibu katika maisha inawezekana hana mtu wakumpa msada wowote Nakumbuka kuna wakati Blog ya Mjengwa alitembelea sehemu moja ya Tanzania akamkuta dada mmoja anawasaidia watoto wadogo kusoma na kuandika lakini hakuwa na nyezo pia alikuwa anafanya vile kwa huruma zake tu Mjengwa alipoweka ile habari na maelezo aliyoyapata kwa yule |Dada walitokea wasomaji wake wengi kutowa msada kwa vifaa kwa wale watoto na yule dada aliyekuwa anawasaidia pale mtaani naimani kama kungekuwa na maelezo zaidi zidi ya huyu dada muosha vioo kungetokea wengi kutowa marifa nini kifanyike ili aondokane na hali hiyo (Tenda wema Wende zako Usingoje Shukurani)
    From :Toufiq Mchambawima

    ReplyDelete
  14. Mara zooote Vijana waoaji mnakimbilia mademu waliokuwa au waliokaa Ki Miss miss na Watoto wa Kimjini!, mnaacha vifaa vya kuwapeni uhakika wa maisha kama huyu Msichana.

    Vijana mnajali sana mwonekano na Matanuzi ya muda badala ya dira ya maisha ambayo ndiyo muhimu sana kumpata mtu aliye tayari kwa shida na raha.

    Mnaona Wasichana waosha kucha na miguu na wapaka poda huku wakitumia kwa sana bidhaa za Mchina kama kope na nyusi ndio wanafaa,,,kumbe lohhh mnakuwa mmekali kuti kavu huku hela yenyewe Laki Nane Tsh.800,000/= mlizopata ikiwa ni ya Gemu la Msimu!, ile kipato kikiyumba ohhh anakula kona sio mwenzako tena!

    Sasa mnaonaje, mfano wewe Kijana siku Mipango imekataa kabisa Kazini au Maskani kwako na umerudi kwa mguu nyumbani, ukiwa na Jembe kama hili jiko lenu litalala paka?

    ReplyDelete
  15. Mhe. Raisi Kikwete,

    Hongera kwa jitihada kubwaaa sana kwenye kasi ya mabadiliko ya kiuchumi.

    Ni muda sasa wa kuharakaisha na kutafuta uwezekano wa kuondokana na ajira zisizo rasmi kama hii, kama mambo yetu yatakuwa na mwelekeo Binti huyu atajikuta amerudi kwao Lindi ama Mtwara akisafisha Mabomba katika Mitambo ya Gesi na Mafuta kwa angalau mshahara wa juu kuliko kuosha kwa bei ya Tsh. 1,000 kwa kila gari vioo vya magari ya Mabosi Jijini Darisalama!

    ReplyDelete
  16. Mdau wa kwanza, kuosha magari vioo hata huko UK wanafanya na ombaomba pia wakizungu wapo, je kwanini na UK nako kuna watu kama hawa. Maisha ujanja kama wewe mwenye unayefanya Mitkasi UK!!

    ReplyDelete
  17. Ya nini tabu niende Majuu au Masauzi nikafanye kazi Ugenini kwa mchaka mchaka tena kwa vibali?

    Si, bora nibakie hapahapa nyumbani Bongo Dispilini ambako uwezekano wa kula yako kwa mkono kwenda kinywani unatokana na wepesi wako katika kujituma na kujikataa wanapotokea watu kama Mgambo wa Manispaa?

    Mhe. Raisi wetu ni bora hii Sekta isiyo Rasmi ichelewe kufungwa!

    ReplyDelete
  18. Ama kweli Bongo uwezekano bado ni mkubwa!

    Nchi zingine huwezi kukurupuka kwako uende barabarani na Kopo mkononi na Tambara ukaanza kuosha vioo vya magari.

    Asalaleee, si utasikia rungu la Mgongo ukazimia na ukizinduka ukajikuta zamaaani upo ndani Lupango?

    ReplyDelete
  19. Wamajuu Madiaspora,

    Golden chance kama hii mnayo huko?

    Mtu unadamka na ji ndoo lako la maji na tambara mkononi unawahi barabarani unavuna fedha bila Kodi wala kutakiwa vibali.

    Ahhh wapi, Majuu hakunaga kama hivi, huko kama ni Kazi za Magendo mnafanya Usiku, kwa Majina ya Bandia au kwa kujificha ficha au ndani ya Magahala ya giza bila taa!

    ReplyDelete
  20. kwa kweli hii picha ya huyu dada imenisikitisha sana, Mungu akusaidie mdau hapo juu kwa wazo lako zuri,jinsi ya kusaidiana wabongo hivi sasa ni issue nzito, akisaidiwa huyu utaona wanavyokuja wengi kwa njia hiyo, ni hayo tu

    ReplyDelete
  21. By mitkasi uk ebwana mungu akubariki na akujaliye kila la kheri wewe kweli mtu na una utu nimesoma comment yako na ikanigusa ile mbaya, uliyosema ni yote sawiya kabisa watu kazi yetu kuingia katika mitandaoni kusoma vitu na baadaye kusikitika au kufurahi na kutoa comment za utumbu utumbu bila kuonyesha nia ya kumsaidia muhusika yoyote yule aliye na matatizo kwa kweli toka niingiye katika mtandao wa michuzi na minginewe sijaona mtu akaitoa comment nzuri na yenye hekma na busara na yenye imani ya kutoa na kumsadia kama yako kwakweli nakufagilia sana mitkasi uk.

    mdau los angeles

    ReplyDelete
  22. Jamani tujadili namna ya kuwakomboa vijana. Huyu binti hastahili kuwa barabarani anatakiwa awe darasani lakini badala yake tunaleta ushabiki hapa. Naomba mlete suluhisho badala ya kuweka siasa hapa, Deo.

    ReplyDelete
  23. we mdau wa Sweden useme kweli jamani eh KWA TAARIFA YENU SWEDEN MWANAMKE NI DILI HUPATI MWANAMKE KABISAA LABDA VISEE-ILA WANAWAKE WA NYUMBANI WOTE WANAJIOZA KWA MIDUME YA KIZUNGU WAO RAHISI KUPATIKANA NA WAZUNGU LAKINI SI KWA WAAFRICA WENZAO WANAJIONA WAO WAZUNGU ZAIDI SASA KAMA UMECHOKA KUPIGA P...TO SEMA TU UNATAKA MKE UOE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...