Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifwamba akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii Vitalis Maembe akionyesha mfano atakavyokamua siku hiyo.
Dude akitoa kionjo cha nyimbo yake atakayoitambulisha kwa mara ya kwanza siku hiyo.
Baadhi ya wasanii hao wakisikiliza mawaidha kutoka kwa rais wao.
Waandishi wa habari wakichukua matukio ya ishu hiyo.

RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifamba, leo amezungumzia juu ya maandalizi ya tamasha la wasanii wa filamu Bongo, walivyojiandaa kwa makamuzi ya nguvu Jumamosi hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya wanahabari, katika viwanja vya Leaders Club leo, Mwakifwamba alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na kila kilichopangwa kitafanyika. Katika upande wa burudani, kutakuwa na wasanii mbalimbali waliojitolea kusapoti tamasha hilo ambao ni Vitalis Maembe, Mrisho Mpoto, Scorpion Girls, Dude, Mtunisi, Radon, Ray, JB, Wema, Jack Wolper, Uwoya, Dk Cheni, na wengine kibao.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...