Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima ili azungumze na Maafisa wa Jeshi hilo kabla ya uzinduzi wa magari ya 10 ya kuwasafirisha Mahabusu mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza katika hafla ya uzinduzi wa jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima akiwa ndani ya moja ya Basi la kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani mkoani Pwani.
Sehemu ya magari 10 ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima katika hafla iliyofanyika Gereza la Mahabusu Ubena mkoani Pwani.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (Kushoto) akitoa ufafanuzi zaidi kwa waandishi wa habari kuhusiana na magari 10 yaliyozinduliwa mkoani Pwani.
Mzee Minja, nunua na Matrakta, vijana wakajifunza kazi za Kilimo na Kuzalisha. Hao ni rasilimali kubwa sana ya uzalishaji. Itumie kikamilifu
ReplyDelete
ReplyDeletekazi nzuri,
tunaomba hawa wenzetu waboreshewe na mazingira wanayoishi,chakula na kuheshmiwa utu wao. ni wenzetu,ndugu zetu, rafiki na jirani zetu.
Kamishina Mkuu Mhe. John Minja, Watanzania tutafarijika sana, sana, sana kama Mabasi hayo watapanda wale Wezi wetu Waheshimiwa wa Mabilioni ya Shilingi na sio Wezi wa Kuku na Simu za Mikononi!
ReplyDelete