Habari zilizotufikia punde zinasema vurugu zinaendelea mjini Mtwara ambapo leo wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya Nyumba ya Mhe. Hawa Ghasia Waziri wa Tamisemi na ya Mhe. Mohamed Sinani Mwenyekiti wa CCM mkoa zilizopo mtaa wa Sinani.
Wakiwa katika mahakama ya mwanzo Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka kituo kikuu cha mabasi na soko kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi. Baadhi ya barabara za mji huo zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi…Bado haijajulikana chanzo ama sababu ya vurugu hizo, nasi tunafuatilia kwa karibu n tutawapasha yanayojiri kwa kadri tutapopata taarifa

![]() |
Baadhi ya watuhumwa wa vurugu hzo wakiwa chini ya ulinzi |
Tatizo nini??Tutibu tatizo,mimi siombi itokee lakini wananchi wakiamua hayo mabomu ya machozi hayawezi kuwazuia kufanya watakalo.Kuna tatizo katika mfumo wetu na inabidi Serikali ifanye kazi ya ziada,mara leo bodaboda mwanza wamefunga barabara,mara Ikwiriri wachoma kituo cha polisi,mara sijui nini.Kuna rafiki yangu alishawahi kuandika humu kwenye blog ya jamii kwamba Mbuyu ulianza kama mchicha.
ReplyDeleteDavid V
Bado tunaelekeza mitutu kwa raia wasio na silaha?Hatujifunzi?
ReplyDeleteangalieni isije ikawa kuna mkono toka nje - uamsho, alshabab, boko haramu n.k.
ReplyDeleteHivi itamsaidia nani kuchoma moto mahakama na nyumba za watu? Tatizo hapa ni uwezo wa kufikiria ni mdogo mno! Sasa leo unachoma moto mahakama, chombo pekee kinachosimamia haki, na mtu aliechoma moto akikamatwa ataenda kujitetea wapi? yaani this is too much hio mahakma ndio ilioamua gesi iende dar?
ReplyDeleteMdau ulosema khs Uamsho na Alshabab ww ni mdini na huna maana na yoyote na una chuki na Uislam na Waislam, nashangaa kwanini Michuzi kaiachia comment yako wakati zetu huwa anazibania.Mbona kwnye vurugu za CHADEMA Arusha,Bodaboda Mwanza etc hujasema khs mkono wa Wagalatia?Wacha ujinga ww na kuamini conspiracy theoeries,kuwa japo na akili ya samaki yakuweza kupambanua wapi lilipo tatizo.
ReplyDeleteNa ww unaesema watu wanachoma mahakama kwa sababu uwezo wao mdogo wakufiria nakuuliza hivi kwanini hawakuchoma Bar,Stendi ya mabus au Soko?Haki gani inayosimamiwa na kutolewa na mahakama za Bongo?Acheni kuwa watumwa wa fikra,mm sitoki Mtwara lkn huu mgogoro unaonesha namna watu wa mkoa huo walivyopoteza imani na serikali pamoja na idara zake zote.Na hizo nyumba zilizochomwa ni za Viongozi kwanini hawakuchoma nyumba za wauza miogo?
Ni hatari lakini polisi wameanzisha!
ReplyDeletemiaka yote ya uhuru walisauliwa leo mnataka kuchukua mali yaho ,hata mie sikubali maendeleo yaliletwa kaskazini na kusini kusahulika wekeni viwanda na wao wapate hajira na kufurahia matunda ,shinyanga na mwanza madini ya uko yameleta nini ?
ReplyDeleteWe uliyefikiria mambo ya udini ndo unaleta udini sasa, mambo yapo wazi wanaohamasisha vitu kama hivyo ni hayo makundi aliyoyataja huyo jamaa hapo juu then we unasema mambo ya udini how?? Kuna mtu dunia hii asiyejua hayo makundi yanajishughulisha na nini? Je ni kosa kuwataja? wakati mwengine hakuna haja ya kutaka kuleta chokochoko kwenye mambo mepesi kama hayo jitahidini kutumia akili hata kama unaelimu DUNI
ReplyDeletesuala ama chanzo ni hili neno lenye herufi 4 tu yaani G.E.S.I
ReplyDeleteKwa kufikia Kuunguza 'Mahakama ya Mwanzo' (SIO MAHAKAMA YA RUFAA AU MAHAKAMA KUU) na kutumia Mabunduki badala ya kutafuta suluhu ya suala la gesi kistaarabu, kazi ipo!
ReplyDeleteJamani tuseme kila kitu lakini kuchoma moto mahakama na kuvunja na kuiba vitu kutoka nyumba za viongozi hawa kwa kisingizio eti gesi, haikubaliki hata kidogo. Mimi ni mzaliwa wa Mtwara, na ninajua watu waliofanye mambo haya ni watu wachache na wanachafua jina la wana mtwara. Ajenda yote ya gesi itasahaulika na watu watakuwa wanaongelea fujo hizi.
ReplyDeleteSasa wewe Anony wa Fri Jan 25, 11:23:00 pm 2013, unaona sawa kuharibu mali za watu? Mwenye fikra potovu hapa ni nani. Watu wengine bwana? Hio itamsaidia nani. Na kwa taarifa yako, wawekezaji wengi wa Mtwara washaanza kufiikiria kuondoka! Sasa wewe mwenye uwezo wa kufikiria, jiulize atakae umia hapo nani? Viongozi, Wawekezaji au Wananchi wa mtwara?

ReplyDeletehaa kachero kashikilia kwenye kibonyezeo kabisa hafu akifyatua si jamaa chari haki ya Mungu acheni nyie askari utani na hiyo maneno tumieni ufundi mliojifunza kupambana na watu ambao hawana nguvu kukushindeni nyie msikimbilie buleti.ah hovyo askari wetu.
ReplyDeleteMmh kweli watu wa mtwara wamechoka....tatueni tatizo viogozi wetu
ReplyDeleteKaka Michuzi lete updates za Masasi Mtwara leo hii jumamosi hali ni mbaya sana. Ninasikitika kukupa taarifa kuwa hadi gari la kubebea wagonjwa ambulance limechomwa moto
ReplyDeleteachana na vurugu, tembelea hapa kuona nafasi za kazi zilizopo, http://www.ajiraonline.com
ReplyDeletekwanza kuwepo kwenye eneo la tukio halafu ndio utajua kwa nini polisi wanatumia nguvu!!!
ReplyDeleteMdau ulosema khs Uamsho na Alshabab ww ni mdini na huna maana na yoyote na una chuki na Uislam na Waislam, nashangaa kwanini Michuzi kaiachia comment yako wakati zetu huwa anazibania.Mbona kwnye vurugu za CHADEMA Arusha,Bodaboda Mwanza etc hujasema khs mkono wa Wagalatia?Wacha ujinga ww na kuamini conspiracy theoeries,kuwa japo na akili ya samaki yakuweza kupambanua wapi lilipo tatizo.
ReplyDeleteNa ww unaesema watu wanachoma mahakama kwa sababu uwezo wao mdogo wakufiria nakuuliza hivi kwanini hawakuchoma Bar,Stendi ya mabus au Soko?Haki gani inayosimamiwa na kutolewa na mahakama za Bongo?Acheni kuwa watumwa wa fikra,mm sitoki Mtwara lkn huu mgogoro unaonesha namna watu wa mkoa huo walivyopoteza imani na serikali pamoja na idara zake zote.Na hizo nyumba zilizochomwa ni za Viongozi kwanini hawakuchoma nyumba za wauza miogo?
Fri Jan 25, 11:23:00 pm 2013
Wa UK utawatambua kwa matusi na kutetea udini ilhali hata dini zao zinakataza fujo. haya endeleeni na uchochezi wenu lakini tulishawabaini muda mrefu.
TATIZO LA MTWARA NI UCHUMI:
ReplyDeleteMzozo mzima ni suala la Uchumi na hatima ya maisha ya wakazi wa huko Kusini ambako kumekuwa na jina jipya kuitwa 'makalioni' mwa nchi kutokana na kudorora Kimaisha na fursa za kawaida ambazo wengine nchini wanazo!
LAZIMA TUKUBALI NI KUWA KWA MIAKA NENDA MIAKA RUDI NCHI YETU IMEDUMAA KIUCHUMI KUTOKANA NA UTAMADUNI MBAYA WA 'UCHUMI WA MALIGHAFI' AMBAPO MALI ZETU ZOOOTE KUANZIA KILIMO HADI MADINI ZIMEKUWA ZIKIUZWA NG'AMBO KWENYE MASOKO YA KIMATAIFA ZIKIWA UN-PROCCESSED AU GHAFI AMBAPO KWA KANUNI ZA MASOKO HAYO MALI ZILIZO RAW AU GHAFI HUUZWA BEI YA KARIBU NA BURE:
Sasa leo hii baada ya miaka 51 ya Uhuru wa nchi bado Rasilimali adimu duniani kama Gesi inatakiwa iuzwe ikiwa ghafi kwa bei ya chini karibu na bure!
HICHO NDIO KITU AMBACHO WANA KUSINI NA MTWARA WANAPIGANIA, KWA SABABU WANACHOTAKA NI MAMBO MAKUBWA MATATU (3) YENYE TIJA:
(1.)KUKUZA AJIRA:
KWA KUICHAMBUA GESI BADALA YA KUUZWA IKIWA GHAFI KWA BEI YA CHINI KWANI KUICHAMBUA GESI KUNAZAA AJIRA KWA IDADI YA BIDHAA ZAIDI YA 100 (PETROCHEMICALS PRODUCTS) ZINAZOTOKANA NA VIWANDA VYA MALI HII PAMOJA NA HUDUMA NYINGI ZAIDI ZINAZOAMBATANA.
(2.)KUPANDA THAMANI KWA RASILIMALI ZA GESI (VALUE ADDITION):
WANATOA MSIMAMO KWA MASLAHI YA NCHI PIA KWA KUWA GESI IKIWA PROCESSED ITAPANDISHWA THAMANI NA BIDHAA KUWA FURNISHED OR SEMI FURNISHED AMBAPO ZIKIFIKA MASOMO YA DUNIA ZITAUZIKA KWA BEI ZA JUU ZAIDI NA KUONGEZA PATO LA NCHI, JE, MLIWAHI KUONA ZAMBIA YENYE SHAMBA (COPPER) IKASAFIRISHA MCHANGA WA SHABA KUUZWA NCHI ZA NJE?, HAPANA, NI KUWA ZAMBIA WANA PROCESS COPPER YAO KWENYE MIRABA (COPPER BARS) NA KUFANYA GRADING,QUALITY,AND STANDARDIZING ILI WAWEZE KUUZA KWA BEI ZA JUU MASOKO YAMKIMATAIFA KWA VIWANGO VINAVYOKUBALIKA NA KUKABILIANA NA USHINDANI WA KIMATAIFA.
HIVYO MPANGO WA KUISAFIRISHA GESI HADI DAR NI WAZI HAUTAISHIA KUZALISHA UMEME, INGINE UTAONA INAPANDISHWA MELI NA KUUZWA IKIWA RAW HUKO NJE KWA BEI YA CHINI KARIBU NA BURE.
(3.)PATO LA TAIFA(GDP) GROSS DOMESTIC PRODUCT:
MALI GHAFI YA GESI IKICHAMBULIWA NCHINI KWA IDADI HIYO KUBWA YA BIDHAA AINA ZAIDI YA 100 TOFAUTI TOFAUTI ZITAKAZO ZALISHWA NI WAZI YA KUWA PATO LA TAIFA (GDP) LITAPANDA KWA KUWA GDP INAHESABIWA KWA NJIA KUBWA TATU (i)EXPENDITURE(Matumizi yote nchini ya watu na taasisi)(ii)INCOME(mapato yote nchini za watu na taasisi)(iii)PRODUCT(Uzalishaji wa mali zote nchini uliofanywa na watu na taasisi zote)...HIVYO KUICHAMBUA GESI NCHINI KUTAZAA MAPATO MAKUBWA NCHINI KWA IDADI YA BUDUMA NA BIDHAA ZITAKAZO ZALISHWA KWA KILA MWAKA,KUONGEZA THAMANI YA RASILIMALI KTK UZALISHAJI, KUKUZA AJIRA NA KUKUZA UCHUMI AMBAKO KUTAONDOA UMASIKINI:
HUO NDIO MSIMAMO WA WANA MTWARA JUU YA GESI NA UHALISIA WA JAMBO LENYEWE KAMA TUTATUMIA KANUNI ZA KIUCHUMI NA SIO SIASA, HIVYO KAMA HOJA NI VIWANDA HIVYO HAKUNA HUKO MTWARA SUALA NI KUKOPA NA KWENYE MABENKI DUNIANI NA KUENDELEZA, KAMA SUALA NI UMEME MITAMBO IJENGWE UFULIWE HAPO HAPO MTWARA NA KUSAFIRISHWA UMEME KOKOTE KULE UNAPOTAKIWA, KAMA SUALA NI MAUZO YA GESI KWA NINI ISIPAKIWE KUTOKA BANDARI YA MTWARA KWENYE MELI KWENDA KUUZWA? :
SUALA NI LA KIUCHUMI LINAHITAJI KUTAFAKARI ZAIDI!