Kundi la Wagadu Gu na ngoma yao ya 'Easy Dancing' walikuwa balaa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hili kundi lilipiga Instrumental fulani katikati miaka 80,nadhani 1987.Ile instrumental(Muziki wa Ala) ilikuwa ni noma,highlife Mix.Ankal mambo ya soka rhumba ulikuwa hupendelei enzi hizo?Mambo ya Ole ole..feeling hot hot hot.Usipime

    David V

    ReplyDelete
  2. Assalama Lekko zako Ankali Michuzi!

    Mimi Mdau wa zile za zamani kila siku unanito machozi,

    Nalia, nali ,nalia nalia eee!

    Hapo magoma yanapigwa mimi nikiwa Kijana mdogo handsome boy nikiwa na nywele zangu zote kichwani tena nyeusiii, na sasa nina 'Bandawe' yaani upara kichwani nakata nywele kila siku kipara ili kuficha Uwanja wa ndege kichwani mwangu!

    Nimetoa neno 'Bandawe' hapa watoto wa za kisasa watachanganyikiwa ni kuwa palikuwepo na Mchezaji mmoja anacheza Mpira timu ya Costal Union ya Tanga alikuwa anaitwa TITUS BANDAWE huku akiwa na uhalaza yaani Kipara kichwani kama Bosi fulani hivi!,,,kumbe wala sio bosi ni mtu wa kawaida ila ameangukiwa na neema ya ubosi, wengi wakizungumzia mtu kuwa na Kipara wanaitwa 'Bandawe' kwa jina la jamaa!

    Na mimi sasa ninalo BANDAWE kichwani kama Bosi wa Benki hivi!

    Isipokuwa mimi sikati nywele kipara kwa kuwa 'Bandawe' langu nalitumia kwa Tija kwa mfano kwenye michongo ya kukopa kwenye Mabenki ninakubaliwa Mikopo kirahisi zaidi!!!,,,na wakati wa kuomba kuhudhuria semina za aina kwa aina ninaonekana ni Mchangiaji mzuri kwa muonekano wa kuwa na upara kama msomi fulani.

    Ama kweli ukubwa ni jiwe!

    ReplyDelete
  3. Hehenehehehehe !!!

    Mdau wa pili hapo juu, mimi 'bandawe' pia ninalo linanisaidia lakini kama ulivyosema ukubwa ni jiwe !

    Ninalo bandawe huku nikiwa wala sina kitu!, nina hela ya kula tu kiasi cha mboga.

    Mtihani unakuja unapokuwa ktk nyumba za Ibada ukipitishwa mchango Kofia au Kapu lilipitishwa watu wote wanageuka nyuma wanamwangalia mwenye 'bandawe' anayeonekana Bosi miongoni mwetu inawezekana atatoa chapaa kuokoa jahazi!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili sijuhi nikuite baba au babu maana nina miaka 29, umenichekesha sana na cku yangu haikuwa nzuri leo ila umeibadilisha.
    Ankali cjuhi huwa nakosea wapi kutuma comment maana cjuhi huweki au hazifiki, I hope hii utaweka au imefika.

    ReplyDelete
  5. Ahhh wapi siku hizi watu wenye upara(Bandawe) mbona sio dili kama kitambo,hawatishi tena kama hapo awali, watu wamestukia kua ni kilema tu na sio vinginevyo.

    ReplyDelete
  6. Hehehe!

    Watu tunapishana kimawazo, wapo wanaoamini kuwa watu wenye kuwa na upara kichwani ni moja ya vitu hivi vinahusishwa:

    (i)kuwa na elimu au akili nyingi, (ii)kuwa na uwezo wa kifedha,

    Sasa sijui ukweli ni upi?

    Wadau kazi kwenu maoni!!!

    ReplyDelete
  7. Mdau wa pili, na mimi umenivunja mbavu kama ulivyoibadili siku ya Mdau wa tano (5) kuifanya kwake iwe ya furaha kwa kicheko!

    Mimi pia ninalo 'bandawe' tena kwa balaa zaidi nywele chache zilizobaki pembeni ya kichwa baada ya uhalaza zina mvi kibao!!!

    Nakumbuka nilikuwa Brazameni sana nikiwa na afro langu la nywele kichwani nilikuwa najitazama sana kwenye kioo kwa siku mara kibao!

    Lakini kwa sasa hili lijiupara na mimvi kobwa kobwa kichwani huku uso ukiwa umeniporomoka kama mbuzi hata kioo sikijui!, naweza kukata hadi mwaka sijasalimiana na kioo cha kujitazama, naoga nachana nywele kavu kavu bila kutizama kioo!!!, sasa niangalie nini wakati mimi sio handsome tena na nina makunyanzi usoni ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...