Na Willy Sumia, Katavi

JESHI la polisi mkoani Katavi limetakiwa kubadili utendaji kazi wake ili kujenga imani ya ushirikiano baina ya jeshi hilo na wananchi katika juhudi za kuutokomeza uhalifu mkoani humo.

Hayo yalibainishwa jana na wananchi wa kata ya Kawajense katika mkutano wa hadhara wa polisi jamii uliofanyika katika eneo la Bar ya Web Site iliyoko jirani na shule ya msingi Nyerere katika kata hiyo mjini Mpanda ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi alikuwa akitoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi.

Wananchi hao walilalamikia vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi hilo kutoa siri ya watoa taarifa kwa wahalifu na hivyo kujenga chuki na kuhatarisha usalama wa watoa taarifa na hivyo kudhoofisha juhudi za kupambana na uhalifu mkoani humo.

Wakizungumza wananchi hao waliwasihi viongozi wa jeshi hilo ngazi ya wilaya kuiga utendaji kazi wa aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya hiyo na baadaye kupelekwa mkoani kuwa aliweza kupambana na uhalifu hadi akafanikiwa kuondoa wimbi la ujambazi lililokuwa limeota mizizi wilayani Mpanda.

Akizungumza katika mkutano huo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari aliwasihi wananchi kutokukata tamaa kwa changamoto ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa na yeye mwenyewe tena kwa muda mfupi sana, wanachopaswa kufanya kuanzia sasa ni kumpa taarifa ni askari gani anafanya huo mchezo mchafu wa kiuaji.

Alisema anachoomba kwa wananchi ni kumpa taarifa kwa njia ya simu kwa namba alizozitoa au kumuona popote watakapokutana naye kuhusu matukio ya kuvujisha siri wanazotoa kwa jeshi la polisi ili aweze kuchukua hatua haraka na kwa wakati ili Katavi iendelee kuwa salama bila majambazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya ni Makosa makubwa sana kwa POlisi kutoa siri hizi na kushirikiana na Wahalifu!

    Suala la Polisi Jamii halitakuwa na mafanikio kama Polisi wataendeleza njaa zao kwa kutoa siri kwa Wahalifu kwa malipo ya kibwege.

    ReplyDelete
  2. Hawa waliotoa taarifa ni wapumbavu wa mwisho tena wafukuzwe kazi maana wanahatarisha maisha ya watu wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...