Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walioongozwa na Mwenyekitiwa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba (kulia). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo mstaafu leo ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika leo katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa maoni yake kuhusu KatibaMpya kwaTume. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
Rais mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akibadilisha mawazo na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) na Makamu Mwenyekiti,Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani (katikati). Wajumbe wa Tume walikuta na Rais huyo mstaafu leo ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali ya Tanzania, Mhe. Andrew Chenge akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika leo katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu AugustinoRamadhani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hayo mashati yamewapendeza sana. Hao wote are my favorites! very brave and brightest people in our country. Mzee Mwinyi, Dr. Salim na jaji Augustino Ramadhani hakuna anayewafikia nchi hii.

    ReplyDelete
  2. Mzee Mwinyi mie naomba unipe ruhusa nije kuchuma japo embe moja pale nyumbani kwako Mikocheni kila nikipita pale mate yananitoka kwa ile miembe ilivyo barikiwa kuzaa matunda - pls pls pls

    ReplyDelete
  3. Embe imebarikiwa! Yaani fikra za wengine wetu zina nitatanisha Kapsaaa! Hata umaskini wa watu wetu utasema ni Laana siyo!!!
    Wakati Mzee Mwinyi, anachapa kazi katika bustani yake, hamuoni! Vivyo hivyo wengine wetu tunapofanikiwa kwa kuchapa kazi hanakaa kijiweni kutamani na kupanga namna ya kuja kuchukua buree tena kwa nguvu.
    Kijana, asiyefanya kazi na asile.
    Kwangu niliondoa maua bustani na kupanda miembe na michungwa mbegu ya SUA. Kama wewe, majirani na wapita njia wana nigongea kuomba matunda.
    TUBADILIKE
    Weka mti wa kivuli wenye matunda. Ufaidi mara dufu.

    Mzee Mwinyi, wewe ni mfano wa kuigwa, na wenye busara wanakuiga sana na wamefanikiwa. Hawa wacha waendelee kushusha udenda!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...