Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:

1.      Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila
2.      Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru
3.      Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA
4.      Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba
5.      Majadiliano
6.      Documentary za Regia Mtema
7.      Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema
8.      Chakula cha jioni
9.      Networking



Wasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams

Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820

RMF inawaomba Wanahabari wote wasaidie kusambaza mwaliko huu.

Wasalaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ewe Mwenyezi Mungu,aipumzishe roho yako pema peponi!Ulikuwa Mfano wa Kuigwa,Ulitoa mwanga wa matumaini kwa Waliokata Tamaa!Kazi yako na Idumu Milele kwa wote wenye Mapenzi Mema!Amina!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...