Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.
Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.
Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.
Mwili ukiondoka nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kaka michuzi tunashukuru kwa sisi tulioko makazini kit Kupata nafasi ya kwenda kuzika lakini at least tumeona baadhi ya picha na wenzetu kutuwalkilisha kwenye maziko Wewe ni chum kwani blog nyingi zimelala. Asante sana. Mungu amlaze mahali pema peponi. Regards rt

    ReplyDelete
  2. Ulale pema peponi, Mwenyezi Mungu akuondolee adhabu ya kaburi. Wastara pole sana Mungu akujaalie subira katika wakati huu mgumu. - AMIN

    ReplyDelete
  3. Kuna watu wengine mawenge kweli,huyo mama hapo juu haoni kwamba ummati wote wakinamama hapo msibani wamejifunika vichwa vyao yeye kuacha wazi maana yake ni nini?Hata km si muislam lkn anatakiwa aangalie na kufata watu wanachofanya hapo sio kuleta ukauzu.

    ReplyDelete
  4. Mkaushie ni butwaa tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...