Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kuharibika njia ya reli eneo la Stesheni ya Mikese jana usiku, safari ya treni ya abiria ya kutoka Dar es Salaam kwenda Bara iliyopangwa kuondoka leo Ijumaa Januari 04, 2013 saa 8:30 mchana haitakuwepo.

Taarifa ya siku ya kuondoka itatangazwa baadae kulingana na ushauri wa Jopo la Wataalamu wa TRL waliopelekwa kusimamia ukarabati wa eneo hilo .
Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenzake.
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

IMETOLEWA NA AFISI YA UHUSIANO KWA
NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI –TRL
MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU
DAR ES SALAAM , JANUARI 04, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...