Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu (FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika. 

Pongeli hizi zimetolewa leo na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo kwenye mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoa na watanzania kama wapenda amani barania Afrika. 

Hii ni kutokana na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC/Rwanda na kundi la M23, migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa Sudani na Sudani Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini nay imepongezwa. 

Bunge la Tanzania limewkilishwa na Spika wa Bunge ambaye ameongoza ujumbe wa wabunge watano ambao ni Mhe. Mussa Azzan Zunge, Mhe. Pauline Gekul, na Mhe Sadifa Juma. Wengine ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prudenciana Kikwembe.

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Hemed Mgaza (katikati) Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge na Makanu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulizi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb). Kulia ni Mhe. Sadifa Juma Khamis, (Mb).Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa Wabunge watano kudhuria Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Jukwaa la Kibunge lanchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa PF –ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
Spika Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano huo.
Picha ya pamoja ya maspika, Sekretarieti pamoja washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR. Picha na Prosper Minja-Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tanzania kusifiwa katika kutatua migogoro:

    Tusiishie kujenga kwa wenzetu huku ikiwa kwetu kunateketea!

    Nadhani hazina hiyo ya busara inayotumika huko nje itumike kwa vurugu za ndani ya nchi yetu ingawa nyingi zikihusishwa na misimamo ya Kisiasa.

    Tunataka Suluhisho la kudumu hapa nyumbani ili tuishi raha mustarehe na kujenga nchi kwa Amani na utulivu huku tukiishi kwa kuheshimiana na kushirikiana.

    SHIDA HIZI HAPA CHINI ZIPATE MAJIBU KWA HAZINA YA BUSARA TANZANIA INAZOSIFIWA HUKO NJE.

    1.Saula la Muungano Bara na Visiwani.

    2.Suala la mifarakano ya mara kwa mara kati ya Jeshi la Polisi na Wanahabari, Jeshi la Polisi na Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

    Kwa ujumla suala baya kabisa la Mauaji kwa wasio na hatia ambayo Idara ya Polisi mara kwa mara inalaumiwa kuhusika.

    3.Mambo kama Maandamano ya Wananchi kama huko Mtwara juu ya suala la Gesi.

    4.Mifarakano na mapigano ya mara kwa mara baina ya jamii za Wakulima na Wafugaji.

    5.Vurugu na machafuko na fujo zinazohusihwa na masula ya Kiimani kama tuhuma za Uchawi hadi mauwaji na mifarakano ya Kidini baina ya Wafuasi wa Dini zetu humu nchini kama suala la Mbagala kuhusu Kitabu Kitakatifu (Dini moja na nyingine) na suala la Chang'ombe kuhusu Kiwanja cha Taasisi ya Kidini (miongoni mwa Wafuasi wa Dini moja).

    ZAIDI YA TANZANIA NA VIONGOZI WAKE KUPATA SIFA LUKUKI KUTATUA MIGOGORO HUKO NCHI ZA NJE NI MUHIMU NA SISI WENYEWE KUTATUA KWA HARAKA MATATIZO YETU KWA MIFARAKANO HIYO MITANO (5) HAPO JUU NA MINGINE MINGI, ILI TUPATE NAFASI YA KUTUMIA MUDA KATIKA UJENZI WA TAIFA TUKIPATA MAENDELEO HUKU TUKIISHI KWA AMANI NA UNDUGU NA KUPENDANA KAMA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  2. ...na wakati huohuo, fundi seremala anakalia viti vibovu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...