Kutokana na mahitaji ya muda mrefu ya watalii na watanzania, kupata huduma ya kuwezeshwa kulipia vyumba vya mahoteli na huduma za kitalii kwa njia ya mtandao kwa bei nafuu, kampuni ya Vinjari imeanzisha huduma hiyo kwa kupitia tovuti yake ya www.vinjari.co.tz

Kwa kupitia mtandao wa Vinjari sasa mtu yeyote mwenye kadi ya VISA (iliyowezeshwa kufanya manunuzi kwenye mtandao) na yule mwenye akaunti ya M-Pesa (Tanzania) anaweza kulipia huduma hizo sasa kwa kupitia www.vinjari.co.tz. Huduma hii imetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na kuthibitishwa na taasisi  inayoidhinisha mitandao inayotoa huduma za malipo mbalimbali duniani.

Katika kuperuzi mtandao wa vinjari, mteja ataweza kuchagua aina ya hoteli, mkoa anaotaka kwenda,tarehe anayotaka kwenda pamoja na kiasi ambacho ana uwezo wa kulipia. Mtandao huu kwa sasa unatoa huduma katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha,  Mwanza,  Kilimanjaro, Pwani, Mbeya, Kigoma, Kagera pamoja na Zanzibar.

Vinjari inawakaribisha watu wote katika ulimwengu wa kiteknolojia unaorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali popote ulipo. Pia unaweza kufuatilia huduma za Vinjari kwa kupitia Facebook (www.facebook.com/vinjari) na Twitter (https://twitter.com/VinjariTanzania).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. afadhali ina saidia sana jana tu tulikua tunataka ku book hotel kwa mwezi wa tano.kwaajili ya harusi yetu lakini tulikua hatujui tuanzie wapi maana tupo nje ya nchi na hatujui majina ya hoteli.good job

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...