Luiza Mbutu (kushoto) na mtangazaji wa TBC (katikati) na shabiki wa Twanga, kwa pamoja wakifungua shampeni kuashiria kuukaribisha mwaka mpya wa 2013, na kuuaga mwaka 2012 wakati wa onyesho maalum la bendi hiyo katika ukumbi wa Mango Garden kinondoni,jijini Dar usiku wa kuamkia mwaka huu.

 Mashabiki wa bendi ya Twanga, wakisebeneka, katika onyesho la bendi yao kwenye Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni wakati wa Sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
 Kalala  Junior, akiwachezesha mashabiki wake kwa kusugua kisigino jukwaani.
 Kalala Junior, akiwachezesha wanenguaji wake, na sebene la Twanga......
 Wanamuziki wa bendi ya Twanga, wakipozi kwa picha ya kumbukumbu baada ya kushangilia kuukaribisha mwaka mpya na kufungua shampeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kweli huu ndio ukumbu wa starehe jamani.?Kama banda la kuku kweli kwetu hatujali standard.na hii ndio Bendi yake kubwa Twanga Pepeta African Stars kama vile Simba na Yanga majina makubwa na mashabiki ukuki lakini hamna kitu.Bw.Fedha anaibiwa fedha za klabu usiku akizibeba kwenye fuko la Rambo aibuu .

    ReplyDelete
  2. We mdau unaokandya ukumbi unachemsha kinamna, ukumbi upo poa tu wala hauna noma, watu wanaselebuka hawana hili wala lile,huwa nikija vekesheni bongo sijachagui ukumbi wala nini, mimi naenda sehemu ambayo nitafurahia, ukumbi ukiwa "pasinaa" walalahoi watashindwa kulipa kiingiliom hata huku mamtoni kuna kumbi na kumbi, bendi na vijibendi.

    ReplyDelete
  3. Kweli Banda la kuku :-) lol

    ReplyDelete
  4. Kwani nyiwe mlio majuu mnaendaga kumbi gani za starehe huko?. Huwa SHEREHE ZENU MNAJIFINYA KWENYE VISITING ROOM VYENU HUKU WENGINE WAKIJIBANZA KWENYE CORIDOR ZA NGAZI. Achenu hizo, Mango Gardens pako bomba sana kuliko seemu nying tuu muendazo.

    ReplyDelete
  5. Inaonekana mabo yalikuwa bomba sana hapo. Nilifanikiwa kuangalia live kupitia TBC nikiwa huku UK. Hongereni wazee wa kutwanga na kupepeta kisima cha burudani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...