Sehemu ya watuhumiwa wa vurugu za Mtwara wakikamatwa 
mmoja baada ya mwingine

Hali ya  utulivu  inadaiwa  kurejea katika wilaya ya Masasi  mkoani Mtwara baada ya   vikosi  vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na  polisi  kuungana  kuweka ulinzi huku  watu  zaidi ya 40  wakikamatwa  kuhusika na matukio  ya vurugu za jana.

Mwandishi  John Kasembe anaripoti  kuwa kutokana na vurugu  hizo  waziri mkuu Mizengo Pinda na  waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku  huu wapo Mtwara  wakiendelea na vikao  vya  kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.

Pia inadaiwa  mida ya asubuhi  leo  polisi  walilazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  vijana ambao  walikuwa  wamefunga barabara na  kuwatoza ushuru  batili  wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.

Mbali ya tukio  hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara  kwa siku ya leo shughuli  zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara zimesimamishwa kwa  muda  ili  kukwepa vurugu kama za jana  japo shughuli za ibada  zimeendelea kwa  utulivu  zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. GESI MTWARA:

    Miaka nenda miaka rudi tumekuwa tukiuza nje raslimali zetu kama MADINI, na MAZAO YA KILIMO NA MALI ASILI kama MALI GHAFI NA SIO BIDHAA KAMILI ZILIZOPANDISHWA THAMANI (VALUE ADDITION).

    MFUMO HUO WA RASILIMALI KUUZWA KAMA MALI GHAFI, NDIO PALE UNAKUTA TARATIBU ZA BEI YA KUTUPA KAMA KARAI MOJA LA MCHANGA WA ALMASI AU DHAHABU LINAUZWA KWA TSH.10,000/= TU!!!,

    YAANI BEI SAWA NA BURE WAKATI MCHANGA HUO UKICHEKECHWA NA MALI KUUNDWA INAWEZA KUTOE GRAMU KADHAA ZENYE THAMANI YA JUU YA KIFEDHA KUANZIA KAMA TSH.250,000/= AU ZAIDI!

    Baada zaidi ya miaka 51 ya Uhuru, bado na zao jipya la UCHUMI WETU yaani GESI nayo pia inafikiriwa kuuzwa nje ya nchi IKIWA MALI GHAFI!

    Hayo mahitaji ya kufua umeme Dar Es Salaam hayawezi kutumia gesi yote ya Mtawara, ni lazima ingine itauzwa nje ya nchi haswa kuanzia Kenya kama MALI GHAFI !

    HILI NDILO SUALA LINATIA GHADHABU HATA KAMA MTU SIO MKAZI WA MTWARA!

    ReplyDelete
  2. MPELEKEE KIONGOZI WETU HII COMMENT HATA KAMA UTAIWEKA KAPUNI,

    ISIPOKUWA HISTORIA ITAKUSUTA WEWE MWENYEWE MICHUZI KWA KUWA WEWE SIO JINI KAMA WEWE NA MIMI TUTAKKWENDA MBELE ZA HAKI, BASI KIZAZI CHETU WEWE NA MIMI KITAKACHOBAKI VIJUKUU VYETU VITAPATA TABU KWA UZEMBE WETU, UKILETWA NA KUBANA KWAKO MAONI HAYA WEWE MICHUZI!

    Ni kuwa Mwambie Kiongozi ya kuwa hata wale ambao sio wakazi wa Kusini au Mtwara kwa mwananchi anayeitakia mema inchi yetu na hatima yake atakataa ni vile:

    GESI INAPOFULIWA KWA VIWANDA INAZALISHA AINA ZAIDI YA 100+ ZA BIDHAA AMBAZO ZITAKUZA PATO LA NCHI LA UZALISHAJI MALI ,KUKUZA UCHUMI NA KUONDOA UMASIKINI.

    AINA YA BIDHAA CHACHE ZINAZOTOKANA NA GESI ASILIA:

    -FERTILIZERS
    -SOLVENTS
    -HELLIUM AND BENZINES
    -PLASTICS PRODUCTS AND FOUNDRY
    -TOXICATIONS
    -METHLYNE
    -MOULDERS
    -RENEWABLE ENERGY
    -INDUSTRIAL LIQUORS
    -FURNACES IMPUTS FOR METAL

    (Hivyo mnunuzi wa Gesi ghafi asilia kwa bei ya bure kutoka Tanzania atanufaika na utitiri wa baadhi ya bidhaa kama hizo ambapo nimetaja chache zinafikia zaidi ya aina 100+ )

    NI VILE UCHUMI WA NCHI UNAJENGWA NA IDADI YA THAMANI YA BIDHAA NA HUDUMA ZINAZOZALIHSWA NCHINI HUMO KWA MWAKA HADI MWAKA, HIVYO WANUNUZI WATANUFAIKA ZAIDI YA SISI.

    HIVYO KUUZA GESI IKIWA GHAFI NI SAWA NA KUUZA BEI YA BURE KWA FAIDA ZA KIUCHUMI AMBAZO TUTAZIKOSA.

    KAMA GESI ITAUZWA KAMA MALIGHAFI NI KUWA WATANUFAIKA WATAKAO NUNUA BIDHAA HIYO KWA KUONGEZA UZALISHAJI MALI (GDP) HUKO KWAO KAMA UNAVYOONA HIZO BAADHI YA AINA ZA BIDHAA HAPO JUU, WAKATI SISI TUTAIUZA GESI KWA BEI YA MALIGHAFI YA CHINI.

    PANA TETESI YA KUWA BOMBA LA GESI LIKIFIKA DAR ES SALAAM, LITAELEKEZWA MOMBASA KENYA, HADI UGANDA NA RWANDA, HIVYO NI WAZI MAJIRANI ZETU WATANUFAIKA NA MAZAO YA GESI ZAIDI YA SISI WENYEWE NA KUKUZA UCHUMI WAO (GDP), HUKU SISI TUKIBAKIA HOHE HAHE HAPA AFRIKA YA MASHARIKI!!!

    ReplyDelete
  3. Michuzi Waeleze Viongozi wetu ya kuwa tokea Uhuru tumekuwa tukiuza Mazao yetu ya Kilimo, Mali asili na Madini kwa mtindo wa Mali ghafi.

    Tumeshanyonywa sana kwa Mtindo huo kwa kuwa ktk Masoko yote ya Dunia bidhaa ambazo hazija tengenezwa kwa Upili 'un processed' zinauzwa kwa bei ya kutupa.

    Hivyo na mali kama hii Gesi hatuwezi kukubali iuzwe kama mali ghafi kama mazao ya Kilimo, Mali asili na Madini kama tulivyowatajirisha Mabepari wa dunia miaka kwa miaka, tunataka Viwanda vya ku 'process gas'.

    Mnaweza kutetea ya kuwa Urusi inalo bomba la Gesi kwenda Umoja wa Ulaya, wao wamefanya hivyo kutokana na kuanguka kwa Viwanda vyao baada ya kunaguka kwa Siasa yao ya Kikomunisti hivyo viwanda vya havina vipuli vya kuviendeshea.

    Hawana njia ingine bali kuuza gesi yao Umoja wa Ulaya.

    Michuzi hata ukiiweka hii comenti kapuni, lakini meseji sent.

    Watanzania wenye akili, licha ya kwamba mimi sitokei huko Mtwara hatuwezi kukubali kuwa wajinga kwa kuiuza mali yetu kwa bei ya bureee.

    Tunajua hawa jamaa mara nyingi unakunywa nao chai,,,utawaeleza tu kwa maneno hata kimtindo mkiwa mnakunywa chai!

    ReplyDelete
  4. Hebu mtueleze ,je Zambia jirani zetu na sisi kuwaona wao Mafala wameshawahi kuuza Shaba yao kama 'Mchanga wa shaba' badala ya Miraba ya Shaba?

    Zambia wameamka kwa kuwa ile shaba miaka nenda miaka rudi inapita ikiwa katika Miraba ina maana kazi hizi zimefanyika:

    1-Imewekwa ktk viwango vya ubora kimataifa ili kukidhi soko la ushindani. (Quality control),

    2-Imeweka katika Madaraja. (Graded),

    3-Imewekwa ktk vipimo vinavyokubalika Kimataifa.(Standards),

    4-Imewekwa ktk Jina na Chapa. (Branded),

    5-Imewekwa ktk uthibitisho uliosajiliwa (Certified),

    Pamoja na kuwa mmesema Gas ikifika Dar Es Salaam itatumika kufulia umeme, je iliyobaki itakayouzwa nje mtaiuza ikiwa ghafi au itawekwa katika viwango ili kuipandisha thamani na kuleta mavuno makubwa ya Kipato kama Zambia walivyofanya kwenye shaba yao?

    Kama Gesi mtaiuza ikiwa ghafi tunataka mtuhakikishie taratibu hizo 5 juu zizingatiwe!

    ReplyDelete
  5. Hatuwezi kuiuza Gesi 'KWA BEI YA KULIWA' kama tulivyouza Madini, Mazao ya Kilimo na Mali asili zetu kama mali ghafi.

    Tunahitaji Viwanda ili:

    1-Kukuza Ajira,
    2-Kuongeza thamani ya rasilimali,
    3-Kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi,
    4-Kuondoa Umasikini,
    5-Kuiweka rasilimali ktk usajili maalum ili kuilinda na wezi.

    NDIO HAYO TU, Michuzi na hii weka kapuni ila fikisha ujumbe kwa wahusika,,,la zaidi ukiweka kapuni Wajukuu zako na wa zangu watakuja kutapa tapa maishani baadae!

    ReplyDelete
  6. Kwa suala la Gesi Mtwara tukiwa kama wana CCM safi hatutarajii kukihama Chama chetu kutokana na Msimamo wetu!,

    Kwa nia njema kabisa TUNALAZIMISHA MAPINDUZI YA VIWANDA NCHINI, HUSUSANI MTWARA KWENYE KIANZO CHA RASILIMALI HIYO BADALA KUISAFIRISHA GESI KWENDA DAR ES SALAAM NA KUIUZA GESI IKIWA MALI GHAFI!

    KATIKA ILANI YA UCHAGUZI YA MWAKA 2010 KIPO KIPENGELE CHA MAENDELEO NA HAPA NDIPO TULIPOSIMAMIA!

    TUNAAMINI KWA HAPO NYUNDO YA CHUMA YA CHAMA CHA MAPUNDUZI IMETUA!!!

    ReplyDelete
  7. utulivu Mtwara?

    Bado kwafukuta chinichini, ebo!

    Hawa watu wanataka muendeleze gesi yao ili waachane na adha ya Umachinga Jijini Dar Es Salaam, ili tusilaumiane tena kuwa kwa nini wanakimbilia Jijini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...