Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa Mratibu wa Vituo vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo (Sober House) za Wete Pemba Abdulwaheed Said kwa niaba ya Vodacom Foundation. Wanaoshuhudia ni Menejja wa Vodacom Foundation Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kushoto). Hafla hiyo ilifanyika wkishoni mwa wiki Chakechake Pemba.
Mratibu wa vituo vya kutibu watumiaji wa dawa za kulevya kuacha kutumia dawa hizo (Sober House) vya Wete Pemba Abdulwaheed Said akishukuru kwa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kutoka Vodacom Foundation vilivtolewa kwa Sober House nne za Kisiwani Pemba. Kutoka Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa,Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon. Meneja wa Sober Hosue ya Chakechake Mohammed Kassim na Meneja wa Mahusiano ya Nje Salum Mwalim.Mkabidhiano hayo yamefanyika kwmishoni mwa wiki Mjini Chakecahke.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi dumu la dawa ya kusafishia choo kwa Meneja wa kituo cha kutibu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) cha Mjini Chake Chake Kisiwani Pemba Mohammed Kassim. Wanaoshuhudia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa pili kushoto). Vodacom Foundation imevipatia vituo vinne vya Wete na Chakechake vyakula na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya program yake ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Sehemu ya watu wanaopata tiba ya kuachana na matumiz ya dawa za kulevya katika Sober House za Wete na Chakecahke Kisiwani Pemba wakimsikiza kwa makini Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(hayupo pichani)akizungumza nao wakati Vodacom Foundation ilipofika kituoni hapo kusaidia vyakula na vitu mbalimbali mwishoni mwa wiki. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa.
Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) akishiriki chakula cha mchana na mateja wanaopata tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya katika Sober House ya Chakechake Pemba. Chakula hicho kiliandaliwa na Vodacom Foundation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. mbona huyo bingwa kalipuka hivy?

    ReplyDelete
  2. hebu na mimi munisaidie jamani munachukua vigezo gn kuwapokea hawa ndugu zetu?maana mi mwenyewe nina mdogo wangu wa kiume yupo manyara. ni ameadhirika na madawa na bangi ile mbaya,saivi ni amepiga kimya karibia mwaka mmoja haongei na mtu.nataka apone nisaideni.+255 783 308 037.mubarikiwe.

    ReplyDelete
  3. kaka naona jina la mateja halijakaa vizuri ni bora kuwaita waadhirika wa madawa ya kulevya

    ReplyDelete
  4. Poleni kwa Mkasa mbaya kabisa wa Matumizi ya Madawa!

    Mjitahidi kufuata maelekezo kwa kuwa muhusika binafsi anatakiwa kwa dhati yeye mwenyewe awe ameazimia kuachana na Uteja ndio ataweza kufikia lengo.

    Isiwe baada ya kutembelewa na Vodacoma na kuandaliwa ubwabwa mpevu kabisa wa nazi, mnachomoka mnakwenda chemba na kujidunga tena!

    ReplyDelete
  5. Mojawapo ya kufikwa na Kiyama cha maishani ni Matumizi ya madawa ya kulevya!

    Isipokuwa KANUNI KUBWA SANA MUHIMU KWA WALE WASIPATA ATHARI NA WALIOANGUKA KTK MADHARA NI:

    1.WASIOPATA ATHARI:
    -Usije ukajaribu ama kuonja ladha ya unga, ukijaribu utakuwa umesha kwama na umezama kwenye Uteja kwa kuwa hii kitu ina vitu viwili vikubwa

    (i)DEPENDENCE/ UTEGEMEZI
    Ukishaonja tu, lile shombo lake linanasa kwenye damu yako na unakuwa lazima upate tena , na tena na tena na huwezi kuwa sawa hadi Utegemee mzigo au bidhaa hii kila uchao!...(unga una asili ya gusa unase)

    (ii)TOLERENCE/ MUENDELEZO
    Unga una katabia ka muendelezo, ni kama matumizi mengine ya Ulezi mifano Bangi na Pombe anayeanza huanza kwa kuvuta Msokoto Mmoja ,baada ya muda fulani halewi hadi avute miwili na kuendelea hadi unakuta mtu anavuta Puli au fusho moja ndio alewe!,,,kama Bia Pombe mtu anaanza na Ulevi wa chupa moja mara halewi hadi mbili na kuendelea hadi anafikia halewi hadi amalize Hreti zima ama kushinda kutwa Baa akinywa ndio alewe...SASA MADAWA YANA KIWANGO CHA JUU ZAIDI CHA TABIA YA MWENDELEZO KULIKO BANGI NA POMBE!

    2.WALIO KWISHA POTA ATHARI YA MADAWA:
    -Wanatakiwa waheshimu na kufuata kanuni na maelekezo ya kuachana na madawa , wao wenyewe wawe na nia hiyo kwanza.
    -Wanatakiwa wawe kwenye Ungalizi na wajitenge na watu wa Kundi linaloendelea na Matumizi ya Madawa MFANO JITIHADA ILIYOFANYWA NA MDAU MSIMAMIZI MRATIBU WA KITUO HICHO NDG. ABDULWAHID SAID NA VODACOM FOUNDATION ZINAWEZA KUINGIA DOSARI MARA BAADA YA SHIBE HIYO YA UBWABWA WA NAZI KWA SAMAKI JODARI AMA NGURU, MATEJA WAKIWA HAWANA USIMAMIZI WANAWEZA KUSHUSHA SHIBE ZAO KWA KETA ZA GANJA AMA MADAWA TENA!!!

    ReplyDelete
  6. Maustaadhi Mateja Wastaafu Pemba,

    Uchapeni ubwabwa kwa samaki lakini mkishiba msije tena kushushia kwa mineli ya Ganja na Kete za Unga!

    ReplyDelete
  7. ...Hahahaha Mdau wa 6 hapo juu, kumlinda Teja ama kundi la Mateja ni sawa na kulilinda shamba la mazao dhidi ya Kima, kwa kuwa ukisinzia tu, ohhh wamekula kona wanajidunga tena!

    Ukizingatia wamesha shiba ubwabwa kwa samaki wa nazi tena?

    Kwa nini wasitohoe shibe zao kwa Fantom za ganja na kete za mizigo?

    ReplyDelete
  8. Dunia ina mitihani sana,

    Mojawapo ni matumizi ya madawa kama haya.

    Mungu awanusuru na awaongoze hawa watu waachane na shida hii!

    ReplyDelete
  9. Masikini weee jamaa Maustadhi wa maana na Kofia zao kichwani ila Matumizi ya Madawa yamewaweka pagumu kimaisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...