Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi Agness Hokororo (katikati) akihututubia wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya wachimbaji wadogo wa madini katika wilaya ya Ruangwa.wengine pichani ni baadhi ya viongozi wilayani Ruangwa.
Na Abdulaziz Video,Ruangwa
Wachimbaji wadogowadogo wa madini Wilayani Ruangwa wametakiwa kuacha
kufanya kazi katika mfumo usio rasmi badala yake wabadilike kwa
kuingia katika mfumo rasmi ambao utawawezesha kukubalika na taasisi za
fedha kutokana na kukua kwa sekta ya Madini Duniani ikiendana na
Mabadiliko ya Uchumi hapa Nchini.
Wito huo Umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi
Agness Hokororo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya
wachimbaji wadogo wa madini wilayani hapa ambapo alibainisha
kuwa uchimbaji mdogo ni sekta ya kibiashara ambayo inaweza kuongeza
kipato cha wananchi kwa kuongeza ajira pamoja na uchangia na ukuaji wa
pato la taifa.
Licha ya kutokuwepo kwa taarifa sahihi za uzalishaji na
uuzaji wa madini na wachimbaji wadogo kutozifanya shughuli za
uchimbaji madini kama shughuli maalum ambazo zinaweza kuajiri na
kuajiriwa.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamewezeshwa na Wizara ya Nishati na Madini
na kuratibiwa na ofisi ya Kamishna wa Madini kanda ya kusini na
kuhusisisha Wachimbaji wadogo,Madiwani,Watendaji wa vijiji/kata ambapo
mada mbali mbali zitatolewa zikiwamao za Sheria ya madini ya mwaka
2010,Ufafanuzi wa sera ya madini,Fursa za madini zilizopo Ruangwa na
Matumizi salama ya Baruti ambapo pia watapewa Mwongozo wa kuandaa
mpango wa kutunza Mazingira(EPP0).
Baadhi ya Wadau waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa (hayupo pichani)
Sekretarieti ikiendelea na kazi yake ya kukusanya maoni ya wadau hao.
Picha ya Pamoja.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...