Mshiriki Ally Kawina akikamua.
 
 Martin Gaspar Fundi, mshiriki aliyeshangiliwa zaidi akitiririka.
Jaji wa kinyang’anyiro hicho, Abdallah Mrisho 'Abby Cool' (kushoto), akiwapa somo washiriki (hawapo pichani). Kulia ni jaji mwenzake, John Dilinga ‘DJ JD’.
Mwakilishi wa mkoa wa Mara, Boniface Mirumbe, akionesha uwezo.
Mshiriki aliyeokolewa kutoka ‘danger zone’, Paizo Mussa akionyesha makali baada ya kurudishwa kundini.
 
 MC wa kinyang’anyiro hicho, D 12O, kutoka kituo cha luninga cha DTV, akiongoza mchakato.
---

WASHIRIKI wa shindano la kumsaka mkali wa kuchana mistari ya ‘hip hop’ la The Mic King (Mkali wa Maiki), jana usiku walichuana vikali kutiririka na mistari kwa kutumia neno ‘Mi Mkali’. 

Katika mchuano huo washiriki wawili waliokuwa eneo la hatari la kuweza kuondolea katika mashindano (danger zone), Paizo Mussa amerudishwa kuendelea na mashindano hayo ya kuwania gari jipya la kisasa, na Mohammed Hassan ametupwa nje baada ya kupigiwa kura na mashabiki. 

Mashabiki waliokuwa ukumbini hapo walisikika wakipiga mayowe ya kumshangilia mshiriki, Martin Gaspar Fundi, baada ya kuonyesha uwezo wa juu wa kuondoka na mistari ya ‘hip hop’ kwa kutumia neno ‘Mi Mkali’.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. 'wakali wa maiki'' msemo huo nimeupenda unaelezea hali halisi ya sanaa yao kuwa ni tofauti na wanamuziki.

    ReplyDelete
  2. haki ya nani huyu dj dilunga aliturushaga roho pale bills acheni tu, sijaona dj mkali kama huyu tz nzima, nasema kweli daima fitina kwangu mwiiikooooo. jamaa alikuwa anaunganisha mavitu ya hatari hukai chini unajikuta unadance for 2 hours nonstop dj jd hakunaga kabisa uuuwii enzi ile bills ilikuwa inatisha. alhamisi ladies free sikukosaga nilikuwa narudi home nimelowa kwa jasho utadhani nimetoka gym, DAVID V, ULIKUWA WAPI ENZI HIZO?
    mdau canada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...