Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina Mkonongo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TDL wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Wizara hiyo mapema leo,jijini dar
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina Mkonongo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinywaji cha Konyagi,David Mgwasa wakisalimiana na wanafunzi wanaosomeshwa na Kampuni hiyo chini ya Mpango wa kumuelimisha Mtoto wa Mkulima wa Zabibu unaojulikana kama ‘Zabibu na Shule kwanza’. Jumla ya wanafunzi 30 wanasomeshwa na Kiwanda cha Konyagi na wametembelea jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kimafunzo.
Mmoja wa Wanafunzi,Chipengwa Yohana kutoka shule ya sekondari ya Handali,Dodoma Vijijini akiuliza swali kwa wafadhili wa mpango wa  “Zabibu na shule kwanza” 
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina Mkonongo akifafanua jambo mbele ya Wahabari (hawapo pichani),kuhusiana na mpango wa kumuelimisha Mtoto wa Mkulima wa Zabibu unaojulikana kama ‘Zabibu na Shule kwanza’,shoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinywaji cha Konyagi,David Mgwasa wanaoufadhili mpango huo.
Pichani kati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinywaji cha Konyagi,David Mgwasa akifafanua kwa kina mradi wanaoufadhili uitwao ‘Zabibu na Shule kwanza’ mbele ya  anahabari jijini dar mapema leo,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina Mkonongo na shoto kwake ni Meneja masoko wa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd,Joseph Chibehe ambao ni  watengenezaji wa kinywaji cha Konyagi
====== =====  ======= =========
Mpango huu wa kusomesha watoto wa mkulima unaojulikana kama “Zabibu na shule kwanza” ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 01 Julai 2011 Bungeni Dodoma na  Spika wa bunge la Tanzania, mama  Anna Makinda.

Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha familia za wakulima walio kwenye mkataba na TDL wanafaidia na kazi za wazazi wao kwa kusaidia watoto wa familia hizo kwenda shule, kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaoshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na kukosa pesa za kulipia  ada na mahitaji muhimu ya shule kutoka kwa wazazi ama walezi wao ambao ni wakulima wa zao la zabibu.

TDL itakuwa imewapunguzia mzigo mkubwa na kuwapa wakulima hawa muda muafaka wa kujitatiti zaidi katika shughuli za  kilimo cha zabibu ili kuziwezesha familia zao kujikimu vizuri kimaisha.

Mradi huu ulianza na watoto kumi (10), na mwaka jana tukaongeza watoto ishirini (20) na ni matarajio kuwa mwaka huu idadi ya watoto watakaopewa ufadhili itakuwa wanafunzi ishirini (20), hivyo kufikisha idadi ya wanafunzi wanaosomeshwa na mpango huu kuwa wanafunzi hamsini (50).  

TDL kama kampuni tunaamini kuwa, uwekezaji kwenye elimu na pia kumsomesha mtoto  ni kukuza uchumi wa nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...