Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamuziki maarufu wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha (Kulia), Askofu Ernest Irungu, ambaye ni Kiongozi wa nyimbo za Injili na ni Mkuu wa Chuo cha Vision College of Theology kilichopo London, Uingereza, mama Zest Irungu (mke wa Bishop Irungu) na Bibi. Mwambola, walipotembelea Ofisi za Ubalozi jana. Bwana na Bibi Mbasha wapo nchini Uingereza, wakitokea Amerika kujitangaza na kutangaza Injili.
Mheshimiwa Balozi, Peter Kallaghe, akipokea zawadi ya CD na DVD kutoka kwa Wanainjili hao Dada Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha. Wanainjili hao wakiwa nchini Uingereza, walitembelea Miji ya Glasgow, Chemsford na Reading na wanatarajiwa kurejea Tanzania siku ya Ijumaa 11/01/2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivyo balozi atakutana na watanzania wa UK lini?

    ReplyDelete
  2. Caroline MarealleJanuary 11, 2013

    Hongera sana Flora Mbasha na mumeo kwa kazi nzuri ya kutangaza kazi ya Mungu.

    Nimefurahi sana kumuona Askofu Irungu na Mke wake Mungu awabariki sana mnajitunza vizuri watumishi wa Mungu mbarikiwe sana, Siwezi kuwasahau maana niliyojifunza katika huduma yenu ya kiroho imenifikisha hapa nilipo mimi pamoja na fanilia yangu nawaombea sana Mungu azidi kuwapigania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...