Wakazi wa Kimanzichana wakifurahi wakati mbunge wao alipokuwa akiulizwa maswali ya kumuudhi na na kusababisha kuzungumza kwa ukali kwenye mkutano huo. |
KATIKA
hali isiyo
ya kawaida mkazi mmoja wa kijiji cha Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani
Pwani Rajabu Juma Mkumba, amesema wananchi wa kijiji hicho wameacha kuwapeleka
shule watoto wao na badalayake wanawapeleka
madrasa kutokana na gharama za madrassa hizo kuwa za bei ya chini kuliko
Shule.
Akimuuliza swali mbunge wa jimbo hilo la
Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Adam Malima,
alisema wanashangazwa na kitendo wanachofanyiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Kimanzichana Kusini cha kuwalipisha ada ya Shilingi Ishirini Elfu kwa
motto mmoja anaetaka kuanza darasa la kwanza.
“Mheshimiwa mbunge Mkuu huyu wa shule
anatoa wapi sharia ya kutuchangisha shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kila
mwanafunzi anaeanza darasa la kwanza? Wakazi wa hapa wengi wanaona bora
watotowao wawapeleke madrassa kule kwasababu adayake ni ndogo,” Alihoji
Mkumba.
Lakini katika hali ya kushangaza mbunge
huyo aligeuka mbogo na kuanza kuwafokea wananchi hao na kuwaambia hayo
wamejitakia wenyewe kutokana na kutofanya juhudi ya kujenga shule nyingine
kwani alishawaambia miaka miwili iliyopita kuwa watafute kiwanja ili ijengwe
shule kwakua wao wanaongezeka sana.
“Nakumbuka miaka miwili iliyopita
niliwaambia kwenye mkutano hapahapa kwamba kasi yetu ya kuongezeka ni kubwa mno hivyo tujitahidi kutafuta
kiwanja mapema ili tuwe na shule nyingine lakini hadi leohakuna
kilichofanyika,” Alisema Malima.
Aidha mbunge huyo aliwaambia wananchi hao
kama wanania ya kweli ya kutaka kutatua baadhi ya matatizo yao inawabidi wafanye
ushirikiano wa dhati kwani wenzao wa kijiji Cha Mwalusembe walishirikiana nay
eye wakaweza kujenga madarasa manne kwa siku 45 lakini kijiji hicho kinamiaka
miwili hakijajenga hata darasa moja.
Mkutano huo ulikuwa ni wa ufunguzi wa
kampeni ya uhamasishaji wa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii kwa wananchi
kwenye Wilaya hiyo, ambapo wananchi wengi walionekana kuwa na maswali mengi
yaliyokuwa nnje ya mada na maudhui ya mkutano huo hali iliyopandisha hasira za
mbunge huyo na kuahidi atakwenda tena tarehe 17 mwezi huu kukutananao.
walikuchagua ili utafute viwanja vya shule zoote zitakazojengwa. si kazi ya wananchi bali yako wewe malima.
ReplyDeleteasante sana wananchi wa kimazichana kwanza aanze yeye mbunge kuwajibishwa kwa sababu hawaendi majimboni kwao kazi yao kukaa dar na kula pesa ya bure ya bunge si huyo mwalimu hana kosa mbunge asiwe mkali hafuatilii maswala ya wananchi wake asante wazee wa kimanzichana oyee
ReplyDeleteKama yeye ni mbunge wao ni kwa nini yeye binafsi hashauri sehemu ya kujengwa shule mpya kijijini humo? kuwaambia wanakijiji watafute kiwanja sio sahihi kabisa. serikali kupitia kwake yeye mbunge ndio wanaotakiwa kutafuta kiwanja.
ReplyDeleteWengi wetu sisi watanzania tunakosa sanaa ya kuongea na mabishano ( art of argument, persuasion and reasoning). Utakuta wengi wetu tuna paza sauti na kufokea tunapoongea hasa tukiwa tunatofautiana kifikra. Nimeona sana tatizo hilo hususan kwenye malumbano pale bungeni. Sio kila kitu tunaweza kujifunza kutoka kwa wazungu, lakini Hilo nahisi ni jambo jema kujifunza hasa ukiangalia jinsi wanavyo debate.
ReplyDeleteMdau,
Mnama
Waache wananchi wamsulubu Mh. Mbunge wao, safi sana
ReplyDeleteMadrasa? swafi sana! kesho oh wakristo wanapendelewa!
ReplyDeletenashukuru wananchi wa kimanzichana kwa kuamka.Heko wananchi wengine tuige mfano huo.
ReplyDeletePole sana Mheshimiwa. Unajimbo gumu sana,inaonekana uelewa wa watu ni mdogo sana na hata hao watoa hoja yaonekana wanatoka jimboni kwako. Hawana wanalojua! Wanakijiji wanapashwa kutoa eneo la ujenzi wa shule na si Mbunge. Mbunge na mhamasishaji asigeuzwe kuwa mradi. Tana katoa na mfano mzuri wa kijiji kingine ambacho tayari kwa uhamasishaji wake wameweza kushirikiana na Mbunge wao na kujenga madarasa 4. Sasa mtu mzima kama huyo anasema anampeleka mtoto madrasa badala ya shule ati madrasa ni rahisi, haya tuone hiyo ajira atakayopata baada ya kumaliza na kuhitimu madrasa. Mdau hapo sidhani kama wanamsulubu Mbunge wao kama uonavyo wewe, bali wanaonyesha ujinga wao na wanajisulubu wao wenyewe kwa maisha yao ya baadaye. Mheshimiwa usikate tamaa maeneo kama hayo ndio ya kutembelea mara kwa mara, wanahitaji msukumo zaidi kutokana na uelewa mdogo.
ReplyDelete