Mkurugenzi wa Mad Mad Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeneza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba. 
Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.  

Na Ripota Wetu.

KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza sanaa hiyo hapa nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii  hao ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.

 “Kwa muda mrefu niliokaa London sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili  kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.


“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.

Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa,  alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu,  kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.

Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.

“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.

Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalienamna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu steve nyerere mbona mie sijawahi kuona filamu zake hata moja au hata ile kinyumbani wanaita pati gazeti ya filamu zake alizotoa??Niliwahi kusoma na kuwahi kuona tena kupitia hapa, kuna siku alikwenda kwa Mama maria kwenda kuomba ruhusa ya kutoa filam inayohusu baba wa taifa lakini nayo pia sijaiona, ila ni mshiriki mzuri wa vikao viwe vya furaha na shida.

    ReplyDelete
  2. Ningemsaidia Mama Yasmin Razak kwamba,katika mikakati yake,pia afikirie kuikuza lugha ya kiswahili kupitia Tasnia ya Filamu,eneo hilo lina soko kubwa sana katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati na hata Kusini!Pia ng'ambo Marekani,Ulaya na kwingineko.Filamu inakuwa kwa Kiswahili,chini yake kuna sub-titles in English,French,German,Spanish,Italiano,Greek,Arabic,and all other key international languages,atakavyo amua yeye (producer & distributor)kulingana na soko alilo lilenga.Lakini,changamoto mpya inayo ibuka hapa kwa wasanii wetu,ni kwamba wasibweteke na wala hawajachelewa,waanze sasa kujifunza masomo ya jioni(evening classes)lugha za kigeni kwa kuanzia na zile chache muhimu,moja baada ya nyingine!Ukisha yavulia nguo maji,shurti uyaoge!hakuna namna!Be brave,and give it a try,nothing is impossible under the sun!....(to....y)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...