Wakiwa katika picha ya pamoja watoto ambao ni mapacha watatu, Rehema, Amani na Neema.
 Na Kalisa Kachuchu wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Edwin Rweyongeza, amewaomba Watanzania kumsaidia kuwatunza watoto wake mapacha watatu ili waweze kukua vizuri kutokana na matatizo ya kipato yanayomkabiri.
Rweyongeza, aliitaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na Chakula cha watoto lishe, yakiwamo maziwa pamoja na matibabu ya kuishiwa na damu yanayoendelea kuwa tatizo kwa watoto wake.
 Rweyongeza alisema ukosefu wa kipato unaomsumbua, unamfanya ashindwe kuwamudu watoto hao waliozaliwa Julai sita mwaka 2011 katika Hospitali ya Mwananyamala.
Alisema kutokana na ukosefu wake wa kipato, Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni, ilikubali Rweyongeza apate msaada kutoka kwa jamii, kwa barua yao waliyoandikaa Septemba 14, mwaka 2011 yenye kumbukumbu namba W/WG/2011 na kusainiwa na A.Mbusa.
“Naomba msaada kutoka kwa Watanzania wenzangu na Dunia kwa ujumla ili watoto wangu waweze kupata lishe na kufanikisha maisha yao, maana mimi baba yao kwa sasa sina kipato chochote kwasababu sina kazi ya kuniingizia kipato.
“Kama ningekuwa na uwezo nisingeomba msaada, ukizingatia kwamba watoto watatu kuwalea ni kazi kubwa, hasa kwa masuala ya lishe na matibabu, kama vile maziwa na mengineyo yanayochangia kukua vizuri,” alisema Rweyongeza.
Kwa wenye moyo nahitaji la kumsadia, kijana huyo mwenye miaka 29, alizitaja namba zake ni 0767 646599, 0719 909085, huku akitanguliza shukrani zake za dhati kwa Watanzania wote.
 Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Edwin Rweyongeza akiwa na familia yake kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. jamani huyu naye anatuahibisha kabisaaa yani kijana unanguvu zako na familia yako wanamerereta na hata nyumba unayoishi inaonekana ni nziri tuuuu una ulemavu wa aina yeyote naona unamkufuru Mungu wewe.pambana na maisha hacha kuwaza misahada kijana mdogo.unawachuria watoto na walimwengu wanasema kila anayetafuta bila kuchoka MUNGU amtupi?

    ReplyDelete
  2. Huyu aache upuuzi,kitu cha kwanza alichotakiwa kufanya yeye katika nafasi ya kwanza ni kuacha kufanya ngono uzembe yaani ngono isiyo na kinga, kwa maana nyingine anatakiwa kuvaa kondom kama hazipo aniambie nimgawie kidogo maana ninazo nyingi na mke wake atumie kinga vidonge vinagawiwa bure hospitali.
    Wasituletee maombi ya kipumbavu hapa, tunamengi ya kufanya, kama vile kupeleka wagonjwa India kutibiwa, na hiyo ndo kipaumbele chetu,kuhusu starehe zake asitusumbue.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwa zawadi hiyo nzuri kutoka kwa Mungu. Kwavile ni kijana mwenye nguvu, ni afadhali atueleze amesomea nini ili apatiwe kazi au ni maeneo gani anaudhoefu nayo. Au kama akipewa fedha ni miradi gani anaweza kufanya. Ndio watanzania watachanga fedha kwa muda lakini issue ni kutatua tatizo hilo na utatuzi uwe wa kudumu. Tupo pamoja tutakutumia fedha kwenye Mpesa ila kama kijana tueleze uwezo wako na matarajio yako ili upate msaada wa maana na wa kudumu. Mungu wetu ni mwema hatakutupa.

    ReplyDelete
  4. Mambo mengine ni aibu, ni vizuri ukatafakari kwanza kabla ya kusema.

    ReplyDelete
  5. kijana huyu alishapewa kazi na akakataa.kisa mshahara mdogo.250000.leo hii anaomba msaada?

    ReplyDelete
  6. alishaajiriwa dar live.akatoroka na pesa

    ReplyDelete
  7. Shime watanzania wenzangu tutoe msaada kwa ndugu yetu E.Rweyongeza na Familia yake, kwa kuwa mtoto wa mwenzako ni mtoto wa kwako, na watoto ni wetu sote ktk jamii yetu ya Tanzania!

    Nani ajuaye?, labda mmoja kati yao hao watoto wa 3 anaweza kuwa Kiongozi wetu ama mtu muhimu nchini Tanzania atakayetufanyia mema?

    Tusewe na hulka mbaya ya kuchangishana pesa nyingi kwa Sherehe Pati na Harusi,

    Mambo kama haya kuwekwa mbele kuchangiwa,

    1.Malezi ya watoto kama hawa,
    2.Huduma za afya na matibabu yetu,
    3.Kuchangia Elimu,

    Ndio endelevu yanayostawisha Jamii yetu zaidi na kutuletea Maendeleo nchini kuliko kuchangishana Mamilioni ya Shilingi kwa Masherehe, Harusi na Tafrija!

    ReplyDelete
  8. ANKALI
    MIMI NADHANI UWE NA UTARATIBU WA KUCHUJA BAADHI YA MAOMBI YA MSAADA
    NINAVYOMUONA HUYU JAMAA ANAYEOMBA ASAIDIWE MICHANGO ILI ALEE WATOTO WAKE NI KAMA HANA JIPYA.MTU ANA AFYA NZURI HIVYO HIVI HAONI AIBU KUJA JAMVINI HAPA KUOMBA ACHANGIWE!!!SI ANAWEZA AKAENDA KUBEBA HATA MIZIGO GARIAKOO APATE PESA ZA KUMSAIDIA KULEA WATOTO WAKE!!!NA HATA HAO WADADA WAWILI PICHANI HAWAWEZI HATA KUPIKA MAANDAZI JAMANI WAKAJIPATIA KIPATO!!!MIMI NAONA ANAIDHALILISHA FAMILIA YAKE NA YEYE MWENYEWE.NINACHOJUA MIMI NI KWAMBA AFYA NI MTAJI,NA HAWA WANA AFYA,KWA NINI WASIFANYE KAZI!!!SASA KILA MTU ASIE NA KIPATO AKIZAA NA KUJA HAPA JAMVINI KUOMBA MSAADA WA KULEA WANAWE SI ITAKUWA BALAA!!!!MI NADHANI AJITAMBUE TU KUWA YEYE NI MTU MZIMA HIVYO ANA JUKUMA LA KUJITUMA NA SI KULIALIA.MAISHA HAYAPO DAR ES SALAAM PEKE YAKE,KAMA YAMEMSHINDA ARUDI KIJIJINI AKALIME NA SIO KUNG'ANG'ANIA KUKAA MJINI NA KUANZA KULIALIA PASIPO SABABU

    ReplyDelete
  9. Mbona una nguvu kabisa za kufanya kazi na halafu maisha yenu hayaonyeshi kama mna taabika maana mrs salon kaenda na wote mmepiga soap soap...Mshukuru Mungu sana kwa zawadi hiyo ya watoto acha kuwadhalilisha kabisa eti huwezi kuwatunza. Mie nahangaika kusaka mtoto nikipata kama hao kwa mpigo nitafurahi sanaaa EEE Mwenyezi Mungu nisaidie.

    ReplyDelete
  10. Mimi ni good ideas.Mungu akubariki. Naomba watanzanie mupokee issue kama wazelondo. Kwani nadhani yeye hakutegemea kuwa na watoto wengi lkn Mungu amemupa hivyo ni vyema tu,tumpe support.Mimi nitafanya sehemu yangu pia.

    ReplyDelete
  11. mhh they look healthy and contented!!!

    ReplyDelete
  12. Mdogo wangu alifariki na mkewe wakaacha watoto watatu. Leo hii mmoja kafaulu kwenda shule za kata si St. kama za wenzetu. Anatakiwa dawati, ada, michango kibao na hali hana baba wala mama na ndugu zake wote hawataki kumsaidia sababu baba yao alikuwa mtoto pekee kwa mama yake. Leo hii tuna kituko cha mtu mwenye miguu miwili na mke mzuri na watoto kibao anaomba msamaha. KUFURU. Rudi kwenu watoto watakula ndizi na maharagwe wataishi na utakuwa hulipi kodi ya nyumba, umeme na maji. Wewe ni BIJAMPOLA HUNA JIPYA.

    ReplyDelete
  13. JAMANI VIPI?MIMI NI MWANAMKE NINA WATOTO 6 NIMEZAA MAPACHA MARA MBILI,WANAMIAKA 3 NA WENGINE MWAKA NA NUSU BWANA KANIKIMBIA,NIPO MWENYEWE NINAUZA MKAA SINA KIPATO KINGINE.WEWE BABA KATAFUTE KAZI USIWE MJINGA.NIPO TEMEKE UKINIONA UTANISAIDIA MAANA WEWE UNAHALI NZURI SANA.MDAU ANNA.

    ReplyDelete
  14. huyo anatakiwa kwanza akaanyeshwe watu wenye shida za maisha halafu aambiwe aombe tena huo msaada anaotaka!!!labda kama shida yake watoto wakifika kwenda nursery waende english medium!!!

    ReplyDelete
  15. unajua nyie hapo juu mnaandika coz mnafikiri maisha yanafanana na unaandika utafkir wewe Mungu ya mola ni mengi unataka changia hutaki fungia upumbavu wako mdomoni kwako...we ni ndugu yake au ankuongezea nn au kukupunguzia nn akiomba anakuaibisha kwani yeye mkwe wako??? Muwe na akili sometym maisha ni mzunguko usioujua.

    ReplyDelete
  16. unajua nyie hapo juu mnaandika coz mnafikiri maisha yanafanana na unaandika utafkir wewe Mungu ya mola ni mengi unataka changia hutaki fungia upumbavu wako mdomoni kwako...we ni ndugu yake au ankuongezea nn au kukupunguzia nn akiomba anakuaibisha kwani yeye mkwe wako??? Muwe na akili sometym maisha ni mzunguko usioujua.

    ReplyDelete
  17. ataghafir, jamaa hajaona wenye shida. Kama wengi walivyosema, mbona anaonekana kanawiri sana na familia wana afya, wamevaa vizuri, hakuna nata mmoja mwenye dalili ya kwashakor. wewe huna hela za kulisha watoto wako, lakini una namba mbili za simu, sasa unalipiaje hizo simu. kauze mkaa, kabebe magunia kariakoo, ukurudi Bukoba kuna migomba tele, hutalala njaa. wacha usanii na utapeli kwa kutumia watoto.

    ReplyDelete
  18. Kuna baadhi ya mambo yanaudhi, inabidi huu mtindo wa kuombaomba uangaliwe sana, msiwasimange watu wanaochangia harusi au misiba maana hizo ni HIARI zao.
    Kaka hii ichukulie kama dharura imekutokea, jitahidi kukomaa wewe na mkeo mlee hao watoto, kweli ni mzigo mkubwa lakini ndio watoto wako hao! Raha ya watoto ni kuwalea mwenyewe sio kuombaomba wakati wewe na mkeo mnaonekana ni watu wenye akili timamu na nguvu.

    Tusitwishane majukumu ambayo hayatuhusu, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, KILA MTU ANA MATATIZO.

    Mtoto wa mwenzako ni mtoto wako ni katika kusaidiana kwenye malezi ya TABIA NJEMA NA ADABU, SIO KWENYE KUNUNUA NEPI NA NIDO.
    Huu uzalendo wa kusaidiana kulea kwa kweli ni kubebeshana majukumu ambayo hayatuhusu, KILA MTU ANAYO YA KWAKE KWENYE PICHA TOFAUTI.

    KINA MAMA WENGI TU WANALEA WATOTO WAO PEKE YAO, TENA WATOTO WENGI, WANAWALISHA, KUWAVISHA, NA KUWASOMESHA KWA KUUZA MAANDAZI YAANI BIASHARA YA CHAKULA. NA MIFANO IPO, SASA HUYU OFISA ANAYEKUJA NA " SIKUPANGA WATOTO 3" ANATAKA KUTUELEZA KITU GANI?


    ReplyDelete
  19. First of all I'd like to say congratulations on the triplets. And yes it is very expensive to take care of multiple babies and their needs or greater.than just having one baby..It's sad that people or quick to judge others this was unexpecte..So if you can't help please keep your mouth off of this family. The Bible says you parish for like of knowledge. So do you research before committing.on Gods hide to man.....

    ReplyDelete
  20. Watanzania inabidi tuombeane,binafsi ninampongeza mpaka hapo alipofikia,coz when u have triple babies Mara nyingi huwa na matatizo ya hapa na pale,sasa jamaa amesema watoto wana tatizo la kupungukiwa damu Mara kwa mara,sasa badala ya kuangalia watoto na kusaidia tunamshambulia mzazi,hakuomba watoto watatu kwa mungu Mara moja,hiyo kwa wenzetu wanaojua umuhimu wa taifa la kesho wanasaidiwa naselikari kwa ajili ya twins,triple nakuendelea, ndugu nasikitika sana Mimi kwa hizo roho za chuki na kumshambulia utafikiri jamaa kauwa watoto,au mlitaka ajiue kama jamaa aliyetia kitanzi yeye na mwanae bila hata ushauri na msaada,ikiwa hata kwa ushauri wako tu mungu atakubariki na siyo kumtukana na kuongea kama sio mzazi,kwa mshahara wa tzhaiwezekani labda labda uwe mwizi wa Mali ya umma na kama sio business man I belive

    ReplyDelete
  21. Naomba nimsaidie mdau aliyetuma post. Nadhani amekosea kuwakilisha maombi yake. Kikubwa nilichokiona hapa ni mambo ya msaada wa matibabu ya upungufu wa damu wa mara kwa mara wa watoto, hilo ndilo kubwa ambalo Watanzania wengi wangekuwa tayari kulichangia.
    Tumsaidieni jamani tukitegemea malipo kwa Mungu. Tatizo la ukosefu wa damu kwa mtoto linasumbua sana, sasa yeye anao watatu na wote wana tatizo hilo kwa mujibu wake.
    Najua kuna watakaokuja na solusheni ya kula michicha na rozela, hii ni zaidi ya hivyo vitu. Inahitaji TIBA.

    Shime tumsaidieni.

    ReplyDelete
  22. Heee,
    Kwenye Michango ya Harusi na Pati mnachanga kwa kuwa kuna ahadi ya kuandaliwa pombe na chakula!

    Kwenye mambo nyeti kama haya mnatoa maoni ya kukandia!

    Uungwana ni vitendo wandugu changieni huduma za malezi ya mapacha watatu !!!

    ReplyDelete
  23. Mdau wa tatu (3) anonymous wa Tue Jan 08, 07:36:00 AM 2013

    Maneno yako ni ya busara sana kwa kuwa hapa suala ni kutatua Tatizo la huyu jamaa na sio kutoa excuse/ au dharura na sababu kibao kuwa ohhh hatuchangi, ohhh mbona ana afya njema, ohhh!

    Kama Madau ualivyopendekeza ni kumtafutia shughuli za kufanya ili aweze kumudu maisha na malezi ya watoto....kumbukeni akupae samaki hajakusaidia, ila anayekusaidia ni yule anayekupatia nyavu za kuvulia samaki!

    Haya ni matatizo na la muhimu matatizo hutafutiawa ufumbuzi wa kudumu na sio kutolewa kejeli na vijembe!

    ReplyDelete
  24. NDIO MAANA YA KUITWA BABA HIYO!

    KUWA MWANAUME KAKA! LEA WATOTO HAO! USITEGEMEE MSAADA! NINI MAANA YA KUSEMA HAWA NI WATOTO WANGU???
    WATU TUNASEMA SANA KWA SABABU NA SISI PIA TUKO NA MAMBO YETU HALAFU ANAJITOKEZA MTU KAMA HUYU KUOMBA MSAADA WA KULISHA NA KIVISHA??? HAPO ADA YA SHULE BADO!!! JIPANGE KAKA!!! WEWE MKEO NA HUYO MWINGINE ATAKUWA SHEMEJI NADHANI, HAMTASHINDWA. WATOTO WATAKUWA TU HAO, ACHA KUJIDHALILISHA KWA MTINDO HUU, WEWE NI MWANAUME, MWANAUME WA KWELI HAKATI TAMAA KULEA WATOTO WAKE.

    HAYA MAMBO YANAKWENDA KIFAMILIA ZAIDI, OMBA KWA WATU WAKO WA KARIBU YAANI NDUGU SIO HOLELA HIVI, HII INADHIHIRISHA KUWA UNAKUBALI KUSHINDWA KUENDESHA FAMILIA YAKO MAPEMA SANA. MWANAUME WA KWELI HAKATI TAMAA KWA FAMILIA YAKE.

    KUNA MDAU KAULIZA "KILA MTU ASIYE NA KIPATO AKIJAALIWA UZAZI AJE HUMU KUOMBA SI ITAKUWA BALAA?" MAANA WENGI TU WASIO NA VIPATO WANAZAA, TENA SANA LAKINI WANAKOMAA KIVYAOVYAO.

    ReplyDelete
  25. Wimbo wa Marehemu Omari Omari anayezikwa leo:

    WIMBO: MAISHA HUJAYAJUA,
    1.Usinifanyie visa kwa sababu umepewaaaa x 2

    2.Usinione mpuuzi kwa vile wewe umepataaaa x 2

    3.Maisha hujayaajuaaaaa

    Lolooo , lololooo

    Ndevu amekosa ngo'mbe lakini mbuzi kapewa, kupata ni majaliwaaa

    -----------------------------------
    HUU WIMBO NI FUNZO KWA WANAOMTAZAMA MTU KWA MWONEKANO ANAPOTOA SHIDA NA KUMWONA KAMA YEYE NI MJINGA.

    TUKUMBUKE SHIDA HAINA MWENYEWE, USIMJAJI MTU KWA MWONEKANO, UNAWEZA KUMKUTA MTU AKAWA NA KITAMBI LAKINI ASIWE NA KITU AKIWA MASIKINI WA KUTUPWA IKIWEZEKANA LADBA HATA CHAKULA KWAKE TABU MLO MMOJA KWA SIKU.

    UNAWEZA KUMKUTA MWINGINE AKIWA NA AFYA YAKE KIMUONEKANO ILHALI AKIWA LABDA ANA SUMBULIWA NA SARATANI.

    WENGINE UNAWEZA KUKUTA WAKIWA NA FEDHA ZAO NA AFYA ZAO NJEMA HUKU WAKIWA HAWAJA JAALIWA KUPATA WATOTO KAMA ALIVYOPATA YEYE NDUGU EDWIN RWECHUNGURA.

    ELEWENI SHIDA, LAZIMA TUKUBALI ZIPO PIA TUSIWAONE WENYE SHIDA KAMA HAWANA AKILI, AMA KUFIKIRI WANAFANYA UTAPELI PEKEE, SHIDA ZIPO NA ZINAPISHANA KUTOKA MTU NA MTU NA KWA UKWELI HAKUNA BINAADAMU ALIYEJITOSHELEZA KWA KILA KITU, UPUNGUFU AU KUKOSA KABISA NI HALI YA KIBINAADAMU KWA KILA MTU.

    HIVYO, TUJARIBU KULIANGALIA SUALA LA HUYU NDUGU YETU KWA JICHO LA TATU (3) KWA KUWA HATA YEYE MWENYEWE ASINGEPENDA ADHALILIKE KWA KUOMBA.

    ReplyDelete
  26. Ama kweli,nimekubali,Watanzania kwa Kukurupuka hamjambo!Huyu Bwana haombi pesa ya chakula,mbona hata picha zake zinaonyesha kwamba hajapigika kiasi hicho?Maisha ya kawaida bado ana uwezo ya kuyamudu!Kwa kutumia "common sense tu",akili ya kuzaliwa,mtu alitakiwa atafakari kwanza,huyu mwenzetu,ni nini hasa anachokiomba?Ukiwaangalia hao (mapacha ni wawili,watatu wanaitwaje?)vichanga wake machoni,utatambua kwamba wana "tatizo la kiafya!".Huyu mwenzetu anaomba msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu ya watoto wake,ili kuzinusuru roho zao!Matibabu hayangoji kesho,kama ambavyo njaa ya tumbo unaweza kusubiri hata siku mbili,huku ukisukuma siku kwa kunywa maji na kipande cha muhogo au ndizi,upo hapo?au umeshapotezea?Tuwe wavumilivu jamani katika kusikiliza kero na matatizo ya wenzetu!Kama anatudanganya,anajidanganya mwenyewe,kwani,siku hizi hakuna pesa za ziada zisizo na majukumu yake!Ninacho omba,hebu tumtake Uncle,atuwekee sawa hapa Ubaoni,huyu jamaaa,nini hasa tatizo lake,Tumbo?au Matibabu?(chaubishi king'ang'anizi)

    ReplyDelete
  27. ANON WA JAN 10, 02:31:00 PM

    "Rweyongeza aliitaja misaada hiyo kuwa ni Chakula cha watoto lishe, yakiwamo maziwa pamoja na matibabu ya kuishiwa na damu yanayoendelea kuwa tatizo kwa watoto wake"

    IMETAJWA KUWA UKOSEFU WA KIPATO UMEMPELEKEA KUOMBA.

    ReplyDelete
  28. Tunahitaji mabadiliko kimtazamo!

    Kuchangia HARUSI,TAFRIJA NA PATI tena kwa Mamilioni ya Shilingi, kwa ajili ya (ulevi na anasa ya kula kwa siku moja) hiyo ni sawa lakini kuchangia Huduma za Malezi kwa watoto na familia iliyo ktk matatizo ya Ndg.Edwin Rwechungura inakuwa hapana?

    Tuache ile hulka ya kulaumiana na kejeli, tuzingatie kwanza uzito wa tatizo kuwa,

    (i)Malezi sio ya mtoto mmoja ni watoto watatu.

    (ii)Watoto wakiwa na tatizo la Kiafya hali ya kupungukiwa na damu ambayo mara zote huleta homa za mara kwa mara.

    (iii)Ieleweke hali yetu halisi ni tete hasa kwa rika alilonalo ndugu yetu Edwin Rwechungura inawezekana ndio kwanza si muda mrefu tokea ahitimu Masomo huku akiwa hata kazi ya kumpatia Kipato cha uhakika hajapata!

    SASA JE, KWA SABABU HIZO 3 HAPO JUU, KWA NINI TUNAMLAUMU SANA RWECHUNGURA NA KUTOA KEJELI BADALA YA KUTAFUTA SULUHISHO LA KUDUMU, AU ANGALAU KUTOA MAWAZO YA MCHANGO JUU YA HALI HII AMBAYO ENDAPO INGETUFIKIA HATA NA SISI (WEWE NA MIMI) PIA TUNGEWEZA KUWA KTK CHANGAMOTO?

    ReplyDelete
  29. Wajameni Ibada haziishii katika kuta nne za Majumba ya Ibada!

    Hapa kwenye Msaada huu wa familia hii ndio sehemu za kuchukulia thawabu za bureee,

    Ibaada haishii kwenye Swala peke yake, tunatakiwa tutoe misaada pia!

    ReplyDelete
  30. Tujitahidi kuwa na busara na pia kujenga uwezo wa Kutatua matatizo sisi wenyewe.

    Hili sio suala la kufikishwa kwa Mhe. Raisi Kikwete tunaweza kujipanga kuanzia hapa jamvini, angalau kwa kurusha chochote ktk Namba hizo za simu.

    Tutowe Michango, tutafute ufumbuzi wa kudumu na ikikosekana pia mchango wa mawazo unasaidia.

    Sio mchezo malezi ya watoto watatu kwa mkupuo tena wakiwa na afya tete !

    ReplyDelete
  31. Inaonekana Mfumo wa Maisha ya Kibepari ya kutokujaliana tumeyaingia kwa kasi ya ajabu!

    Watazania tunakwenda wapi sasa?

    Hatukutokea kwenye maisha ya kindugu ya Ujamaa?

    Tungetegemea tatizo la mwenzetu Ndg.Edwin Rwechungura litatazamwa kwa Darubini ya Kiujamaa kama Msingi wa Maisha ya yetu yalivyo asisiwa na Maisha ya Ujamaa, na litatuliwe kwa pamoja kama wanandugu na sio kutoa Maoni ya kudai kila mtu aubebe mzigo wake wmenyewe.

    Simba anaunguruma wakati wa Mazungumzo ya Habari enzi za Raisi Hayati J.K Nyerere.....

    ....Ngrrrrrrr, ngrrrrr, ngrrrrr, hatuwezi kuishi na mwenzetu kama ndugu, huku mwenzetu akiwa mkali kama Simba, huku nguvu zake dhidi ya wanyonge zikizingatia , urefu wa makucha yake na ukali wa meno yake, Ujamaa, ni utu, utu, utu ,,,,Ubepari ni unyama, unyama, unyama!

    Ama kweli Ujamaa ni utu na Ubepari ni Unyama!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...