Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na Walezi wa Kituo cha watoto yatima cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kituo hicho,mjini Dodoma na kutoa Msaada wa Luninga kwa ajili ya Watoto hao yatima.kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Kituo hicho Fr Vicent Boseri na anaye fuatia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa (TAMISEMI),Mh. Hawa Ghasia
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Fr Vicent Boseri pamoja na msaidizi wa Vicent Sistar Rozaria ambao walimshukuru waziri mkuu kwakukumbuka watoto yatima hapa nchini.Picha na Chris Mfi
Yaani ka-tv tu au kuna msaada mwingine, waziri mkuu mtu mzito bwana..........
ReplyDeleteAcha maroroso wewe! Ati "Yaani Kat-tv...." wewe umetoa msaada gani katika jamii yako, au kazi yako ni kupiga wengine madongo? mtoaji yeyote yule anaelwewa ya kwamba kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
ReplyDelete-mtu hachagui zawadi.
-Mtu akimpa maskini kichache, Mungu humruzuku kingi!
-Mkono utoao ndiyo upatao.
-Kondoo wa bure haaingaliwi meno.
-Cha kupewa kitamu.
Nakdhalika.
Mdau mamtoni > 22 years
and one more from me mdau mamtoni.
ReplyDelete"Akupaye mfupa, kakuwazia"