Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
 Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B',  Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
 Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
 Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
 Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
 Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
 Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
 Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzindzi huo
KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo wakati wa uzinduzi huo
 Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
 KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee,  kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani
 J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
 Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
 BAADAYE: Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
 Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini
 Kariati akionyeshwa maeneo yaliyoathirika
Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzindizi wa Kampeni ya kilimo kwanza na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha zote na Bashir Nkoromo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. mapozi shambani wapi na wapi... hawa wanatuharibia jamii yetu na nywele zao za bandia......

    ReplyDelete
  2. Vijana si mmnaona kilimo-kwanza inalipa, basi wekezeni ktk matrekta badala ya vibajaji, ma-VX 4X4, teksi bubu n.k
    Mdau
    Mwanakijiji

    ReplyDelete
  3. wema ndio nani

    ReplyDelete
  4. WEMA NI MKE WA KANUMBA.

    ReplyDelete
  5. Wazushi tu hawana maana yoyote..watu wanaofanya mambo yakipuuzi na ya aibu ndio wamekuwa wa maana zama hizi..mbona hatujawaona kwenye picha ya Dua au wao hawaamini Mungu.
    ngekua jambo la maana sana km promotion kama hizi wengepewa watu wanapata alama za juu kwenye mitihni ya kitaifa au wanaopata GPA za juu kwenye vyuo vikuu ili kuwahamaisha vijana kupenda shule lkn promotion zimekuwa kwa mamiss,wanamuziki,waigizaji na upuuzi mwengine..sasa mnajenga taifa gani?

    ReplyDelete
  6. Basi wangevaa kuonesha wapo shambani hasa, sasa mavazi ya kutokea wao ndiyo wametinga shamba, sasa hapo mfano uko wapi? Mngewavalisha maovaroli na mabuti.

    Hii nayo imekaa ki-2015-15 hivi

    ReplyDelete
  7. hovyo mbona hao wanakijiji hawajavaa maovaroli na mabuti wivu tu

    ReplyDelete
  8. Shambani...... Unavaa unafikiri unaenda kwenye premiere ya movie ni ajabu sana. Ila sio kosa lao ni uelewa mdogo walipupata wakiwa shule

    ReplyDelete
  9. Hell,it was an impressive Launching!Nawapa pongezi Wasanii wote walioshiriki katika uzinduzi huo,Kwa Mh.Diwani mwenyewe kwa kuja na wazo hilo na kwa kuwa mstari wa mbele,na kwa Waz.Membe,mlezi wa kijiji hicho ambaye najua alishiriki kikamilifu katika maandalizi yote,bila kusahau,kwa Wakazi Wote wa kijiji cha Kwadelo,hususan,Vijana wenyewe,nguvukazi tegemeo la kijiji, na Taifa kwa jumla!Inataka Ujasiri kufanya mambo kama haya,sio mchezo!Vijana zindukeni,wakati ndiyo huu!Kesho Haipo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...