Timu ya Umoja wa Vijana  waendesha Pikipiki za magurudumu matatu Mkoani Mbeya imezinduliwa hivi katibuni na kupewa msaada wa jezi viatu na mipira toka kwa mlezi wao Mwaka Mwakisu hapo mlezi huyo akimkabidhi jezi mwenyekiti wa bajaji mkoa wa mbeya Iddi Ramadani 
Mlezi Mwaka Mwakisu akimkabidhi mipira mwenye kiti wa bajaji mkoa wa mbeya.

Mlezi wa waendesha bajaji mkoa wa Mbeya Mwaka Mwakisu amewataka wanaumoja huo wa bajaji kutumia vifaa hivyo vya michezo  kuleta mshikamano kwenye michezo na afya zao pia na kuacha kushabikia mambo ya kuleta vurugu na kuvunja amani ya mkoa wa mbeya na Tanzania kwa ujumla  
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha bajaji mkoa wa Mbeya akimshukuru mlezi wako wa kuwasaidia vifaa vya michezo na kuzindua timu yao ya waendesha bajaji mkoa wa Mbeya
Mgeni rasmi akipandisha bendera ya timu ya Bajaji FC kuashiria kuzinduliwa kwa timu hiyo
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Bajaji FC wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbona mmeegemea timu moja tu?

    Moja kwa moja kwa kusoma ishara inaonekana Bajaj ni TAWI LA JANGWANI!

    ReplyDelete
  2. Sasa Bajaj F.C mkikutana na Toyota VX-V8 Land Cruiser au Mpinzani wa karibu TOYO mtasemaje?

    ReplyDelete
  3. UZALENDO mwingine mwanawane?

    Mtakuwa hakumkuwatendea haki wengine, ni wazi watasononeka kichini chini!

    Ina maana wooote waendesha Bajaj mtakuwa ni wana Yanga S.C?, ni kweli hamna wa Simba ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...