Hapa ni Msasani Kwa Warioba katika barabara ya Old Bagamoyo Road ambayo kuanzia kesho itaitwa Barabara ya Mwai Kibaki Road kwa heshima aliyotunukiwa kiongozi huyo wa Kenya na Hlmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kufuatia ziara yake ya kitaifa ya siku mbili itayoanza kesho jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik, barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 10.1 ni kuaniza kwenye mataa ya Moroccco karibu na makao makuu ya Airtel hadi mzunguko wa kuelekea Africana kule Mbezi Beach, mkabara na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ.

Akiongea usiku huu, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Rais Kibaki anatarajiwa kuwasili kesho saa 9 alasiri na kupkewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo usiku atamwandalia dhifa ya kitaifa Ikulu.  Keshokutwa. Alhamisi, Rais Kibaki ataongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa PTA ulioko viwanja vya SabaSaba barabara ya Kilwa Road. Pia atatembelea sehemu mbalimbali atazopangiwa katika ziara yake hiyo ambayo pia ataitumia kuwaaga Watanzania kwani muhula wake wa uongozi utafikia kikomo baadaye mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. This is very stupid! you guys are serious or what??? Kibaki is a dictator. He lost the election and cause more than 1000 deaths. Acheni uzembe wa kufikiri. Kibaki hana hadhi na heshima hiyo.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli sioni mantiki ya kuipa jina barabara hii.
    Kuna Kenyatta road, Kenyatta ni rais wa kwanza aliegombea uhuru wa majirani zetu, hapo inaleta maana. Kwanini tusitumie majina ma mashujaa wetu wa Tanzania na watu mashuhuri kama mzee Morris Nyunyusa au bi kidude?
    Mimi kama mkazi wa wilaya ya Kinondoni napinga ili na nitashukuru kama kuna utaratibu wa kisheria wa kupinga basi mtueleze tuuufanye.
    Huu udikteta sasa mara tutasikia Bagamoyo road inaitwa Michael Jackson

    ReplyDelete
  3. KUna vitu vinasikitisha sana na hata kama post haikuwa approved lakini ujumbe utamfikia hata huyu Ankal wetu.Kiongozi kama KAmbona aliyejitolea sana katika mapambano ya uhuru sijasikia kokote mtaa au barabara ikipewa jina lake.kama tatizo ni ugomvi na Nyerere ? mbona Bibi Titi alipewa heshima kwa barabara kuitwa jina lake ? Watu kama Che Guavara ,Otieno aliyepigani uhuru wa Zanzibar (manake tunaambiwa siku ya Mapinduzi Mzee wetu Karume alikuwa Dar),Tom Mboya,Rais Nguabi wa Congo,Steve Biko,Oliver Tambo,Walter Sisulu,Gamal Abdel Nasser,Chabruma,Abushiri na Bwana heri,Kinjeketile,etc Dar kuna mitaa mingi sana haina majina hasa maeneo mapya kama mbezi,Goba,Basi haya,Luguruni,vituka,Yombo,Maji Matitu,,Kibada, na kwingineko

    ReplyDelete
  4. wanaondoa jina la kutangaza utalii,mnaweka la mtu ambaye wala hatusaidii

    ReplyDelete
  5. Naunga mkono hoja za wadau hapo juu, ukifananisha na mashujaa wetu wa kihistoria na watu maarufu hapa nchini kwa kweli kulikuwa hakuna haja ya kumpa Raisi Kibaki heshima hi na kama ingebidi basi kweli angelipewa mtaa mwingine au mipya. Hii tabia ya kubadilisha majina ambayo tumeyazoea inabidi isimamishwe mara moja.

    ReplyDelete
  6. hahahahaha tanzania bwana!!!
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.tatizo ni viongozi wetu wamesoma kupita kiasi na akili nyingi houndoa maarifa. tusiwalaumu jamani.

    ReplyDelete
  7. Why? Why? Why? For goodness sake. When will we mature up?

    ReplyDelete
  8. Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni!

    Mara kumi, mara kumi,

    Kwani si bora wangempa Hayati Gaddafi aliyetuachia Miradi kibao hapa Afrika ya Mashariki?

    ReplyDelete
  9. Viongozi wa tz ni wapuuzi kwakweli,who is kibaki in tz? yaani kuja kutembea tu ndo apewe heshima hiyo jwa kipi hasa anachokuja kukiletea sifa taifa manufaa kwa hayo maziara yake? huko kwake kuna kikwete road au mwinyi road??? Kunakoelekea sasa mtagawa hata nchi na raia wake.Sijakubaliana na hayo maamuzi ya kipuuzi japo najua wananchi hatuna sauti ya kusikilizwa maoni yetu viongozi wanaamuaga tu na wake zao nyumbani ila watanzania wengi hatujaafiki. Kweli tunaacha kuenzi historia yetu kisa kibaki aiseeeee shenzi kbsa.

    ReplyDelete
  10. Makalio ya sufuria hayaogopi MOTO

    ReplyDelete
  11. Sikubaliani na hilo, kwa kipi barabara hiyo inapewa jina la Mwai Kibaki, acheni uzembe wa kufikiri....Kwa heshima gani kubwa aliyokuwa nayo? kwa ku-lose election na kusababisha vifo nchini kwake?
    Still achaneni na mambo ya kuabudu vya watu, kwani sisi hatuna viongozi wenye Sifa, Si ni bora mngeita 'Muhidin Michuzi' road. I, very loudly sau, this is very stupid'

    ReplyDelete
  12. jamani hii sio sawa kabisa, tuache kuita majina ya nchi yetu tunakimbilia ya nchi zingine, yani haina maana kabisa. Kupewa old bagamoyo road ilikuwa na mana yake, sasa mwai kibaki. Je unaweza kutoa justification za msingi za kubadili jina hilo? wanatanzania tunapoteza uasili wetu kwenye kila kitu ili iweje? Kumfurahisha huyo Rais? Hii ni kali ya mwaka, ondoeni hilo jina na shirikisheni wananchi na sio mtu mmoja anakaa na kuamua mwenyewe na maamuzi yake sio sahihi!

    ReplyDelete
  13. Mbona Tanzania tuna viongozi wengi tu au hata macelebrity ambao wameipa sifa nchi yetu, mf Kikwete, Malecela na viongozi wengine, macelelbrity km Kanumba, Remmy ongala is better than this Kibaki to have the name of such a big Road. for me is a big NO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...