BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapongeza waandaaji wa tamasha la kila mwaka la Pasaka, Msama Promotions kwa kulifanya tukio hilo kuwa la kimataifa kwa kushirikisha waimbaji kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza hivi karibuni katika tathimini ya tamasha la mwaka jana lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Basata Ilala jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mfuko wa Uwezeshaji, Angelu Luhala alisema inapendeza kuona jambo hilo linakuwa la Afrika badala ya Afrika Mashariki kama ilivyo hivi sasa.
Luhala alitaka waandaaji hao kuongeza umakini na kuongeza waimbaji kutoka mikoa mingi zaidi tofauti na sasa kwa vile linavuta hisia za watu wengi katika muziki wa Injili wenye maushui ya kumtukuza Mungu.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa, Nsao Shalua licha ya kuipongeza kampuni hiyo ya Msama Promotions kwa ubunifu wa tukio hilo, pia aliisifu kwa kuzingatia sheria na taratibu za baraza hilo ambalo ndio dira ya sanaa Tanzania.
Aliwataka kuwasilisha mapema tathimini ya maandalizi ya mwaka jana ili kufanikisha tamasha lijalo. Naye shabiki wa tamasha hilo, Eunice Muhandia alisema waandaaji wa tamasha hilo wanatakiwa kuweka umakini katika suala la tiketi kwa sababu mwaka jana ilikuwa shida ndani ya uwanja wa taifa.
|
Home
Unlabelled
BASATA waipongeza Msama Promotions
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...