BARAZA
la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa kibali kwa ajili ya Tamasha la Pasaka
linalotarajiwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari jana kuwa kutokana na kupata kibali hicho maandalizi
rasmi sasa yameanza. “Nilikuwa
Napata tabu hata kuanza kuhangaikia ukumbi ambao tutafanyia tamasha maana mwaka
jana tulifanyia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa bado hatujaamua tutafanyia
wapi kwa sababu ilikuwa hatuna kibali.
“Lakini
hatua ya Basata kutupatia kibali inamaanisha tumepata baraka, hivyo tuendelee
na mambo mengine ya maandalizi,” alisema Msama. Alisema wamepanga siku yenyewe
ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam na siku inayofuata bado wanaangalia
wafanye wapi kwani mikoa mbalimbali imeomba ipewe uenyeji.
“Vipo
vigezo tutaviangalia kwa wanaotaka tuwapelelekee, kama vitakuwa sawa basi
tamasha litafanyika kwa watakaotimiza, lakini kwa sasa Jumatatu ya Pasaka bado
hatujaamua wapi twende,” alisema Msama katika taarifa hiyo.
Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni
Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo
Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la
Glorious Celebration.
Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.
Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...