Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (kushot) akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi huyo amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano na Bunge la Namibia kwani kuna mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
Spika Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Balozi wa Namibia nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa Bunge la Tanzania lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni maeneo yapi ambayo yatawafaidisha wananchi wa nchi mbili hizi. Aliainisha maeneo ya mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele. Na Prosper Minja-Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...