Suluhisho kwa waTanzania wenye makazi ya kudumu ughaibuni wenye nia ya kuja kutembea Tanzania kwa ndugu zao na wanapenda kukaa kwenye makazi yao wenyewe na familia zao

4T TARVEN inaruhusu wapangaji wa muda mfupi katika nyumba ambayo ina vyumba vitatu vyote fitted with AC, hot water heater, Flat screen,nyumba ina unlimited supply of water, kuna generator in case of power failure na vyombo vya ndani (fridge, gas cookers etc )kwa ajili ya kujihudumia; usafiri toka airport ni bure kama unabook kwa siku 7 na kuendelea; ulinzi masaa 24, vilevile bei zetu zinatokana na vyumba utakavyotumia,  pia usafiri utatolewa hadi mlimanicity ( asubuhi ) na kurudi ( jioni ) kila siku bila ongezeko la gharama, kwa wakaazi wa zaidi ya wiki moja kwenye nyumba. kwa watakaotumia chumba kimoja tu ni shilingi Shs 50,000 kwa siku, vyumba viwili ni shs 75,000 kwa siku na nyumba nzima ni shs 100,000 wakaazi wote watatumia jiko, makochi, TV  etc, punguzo litatolewa kwa watakaokaa wiki moja na zaidi


Nyumba ipo Mbezi Louis off Morogoro Road , kwa mawasiliano book thetarvenfourt@yahoo.com pia piga simu +255784312199

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sasa mshikaji wakijua wewe ni wa kuja tena umetoka majuu utakuwa salama kweli? Wengine tukirudi tunataka tujichanganye mtu asijue umetoka majuu. Sasa nyumba ikijulikana ni ya wakuja si tutakuwa tunakwidwa kila siku na kunyang'anywa vidola vyetu tulivyovipata kwa machozi? Mdau, CA, USA

    ReplyDelete
  2. unamaanisha familia moja ikitaka chumba kimoja na ingine ikitaka vyumba viwili kwa wakati mmoja na hawajuani ni utawapangisha wote?

    elezea vizuri kama kuna sharing, je ulinzi wa watu kutoibiana upo pia? I mean wapangaji.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tutapanga kwenye Ms Hotel yenye ulizi atutaki. Kuwa roho juu mdau Europa

      Delete
  3. Wandugu zetu wa Majuu watoa Maoni wa kwanza na wa pili:

    Sera ni kukuza Ajira!!!

    Hapo mtawaajiri ndugu zenu vijana wavulana na wasichan wa Bongo kwa kazi hizi:

    1. Mabaunsa ili kuwapa huduma ya Ulinzi na Usalama.

    2.Wasichana kwenye kufua na kupiga pasi.

    3.Chakula, kama mtahitaji madishi ya Kibongo wasichana watawajibika.

    Karibuni sana mjengoni!

    Karibuni nyumbani Tanzania!

    ReplyDelete
  4. Wadau wa No.1 na No.2 juu

    Itakuwa ni nafasi nzuri mkakumbuka kabali za kibongo mlipokuwa miaka ile hamjaondoka kwenda nje!

    Hamkumbuki kabali ya mbao na misumari Manzese?

    Hamkumbuki vijana wa Keko Toroli na kule Chang'ombe walipokuwa wakitesa na MATOFALI yao ya aina ya FATUMA kuvunjia majumba?

    Lakini msiwe na wasiwasi hivi sasa mambo hayo hakuna Polisi imekuwa makini sana na inashirikiana na Jamii kama Polisi Jamii!!!

    Karibuni, shaka ondoeni!

    ReplyDelete
  5. Mdau wa pili Thu Feb 28, 10:48:00 am 2013

    ...Mnatakiwa muutumie muda mtakao kuwa pamoja muweze kujuana na kufahamiana kwa kupanga wote licha ya kuwa hapo kabla hamkuwa mnajuana.

    ...Mnatakiwa muukumbuke ''Siasa Ujamaa na Kujitegemea'' kwa kuishi maisha ya kuchangia na kuchanganyika!

    Tena ingefaa mkawa mnakula pamoja pia na kukaa pamoja kwa kupanga mida ya hadithi na maongezi na kucheza Mabao na Karata pamoja, kitu ambacho kwa miaka migni Majuu hamkuwa mnakipata tokea muondoke Bongo miaka mingi nyuma!!!

    Kama pana wavutaji mnagongeana sigara !

    Kwa wanywaji mapasiana mabakuli ya Kangara na Mbegge!

    Na kula kwenye masinia badala ya self services zenu!

    Mtapeana hadithi za Mashuleni mliposomea Elimu za Sekondari na Vyuoni, mtapata muda wa kukumbuka JKT Mafunzo ya Mujibu wa sheria ambayo sasa yamerejeshwa tena, kama mlipitia huko,

    Kama mlipitia JKT mtapata muda wa kuimba nyimbo za Mchaka mchaka kama hizi:

    WIMBO WA MCHAKA MCHAKA:No.1
    Pri tekenya ,tekenya Pri tekenya tekenya X 3

    WIMBO:No.2
    Amini akifa , akifa nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba X 3

    Na Burudani za kule zilizojulikana kama Disco!
    Sasa mtawezaje kuikumbuka Siasa ya Ujamaa Kujitegemea ya miaka ile ya 1978 na 1979 baada ya Vita vya Uganda?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...