Katibu Mkuu Kiongozi balozi Ombeni Sefue(Kushoto) akimpa zawadi Bwana Francis Mwaipaja na mkewe wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall jijini Dar es Salaam jana.
Akiongea katika hafla hiyo Balozi Sefue alisema kwa Bwana Mwaipaja ni mtu wa kuaminika katika utendaji wake wa kazi na ni mtulivu na makini.Bwana Mwaipaja amehamishiwa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Bwana Mwaipaja aliyekuwa msaidizi wa Katibu mkuu kiongozi alimshukuru Balozi Sefue na kusema amejifunza mengi ikiwemo kuzingatia muda katika utendaji kazi,kutekeleza majukumu kwa ufasaha na ufuatiliaji mambo kwa karibu.(picha Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...