Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha baada ya kumkabidhi kitambulisho cha Taifa, Msanii Isha Mashauzi,(msanii) akiwa miongoni mwa wananchi kutoka Tanzania Bara waliopewa vitambulisho vyao katika hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa,kwa mara ya kwanza kwa Upande wa Zanzibar,hafla iliyofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu, Zanzibar
Isha upo juuuu dada yangu; hongera jike la simba.
ReplyDeleteAssalam Alaykum Mhe. Raisi Shein!
ReplyDeleteNa mimi Mbonde Diwakile wa Bungu-Rufiji naomba tanfadhali nije Zenjibar ili na mimi unipatie Kitambulisho changu.
Nimefarijika sana na Uongozi wako Visiwani!
Ni uamuzi wa Busara sana uliochukuliwa kwa Vitambulisho vya Utaifa kutolewa kwa watu wa Visiwani kupatia Bara na watu wa Bara kupatiwa Visiwani.
ReplyDeleteWapinga Muungano wasichukulie ya kuwa Vitambulisho vinatolewa kwa misingi ya maeneo wanakotoka au qwanakokaa watu.
Kigezo ni sifa za Uraia na Utaifa wa muhusika lakini Sio Uzanzibar na Ubara!
Palikuwa na maradhi ya Ubara na Uzanzibari miongoni mwetu.
Mmeamini sasa ya kuwa kila maradhi yana dawa yake?
Wapinga Muungano nyuso zimewashuka kama mbuzi kwa tukio hili la Isha Mashauzi wa Bara kupata National ID Visiwani.
ReplyDeleteItawauma saana, itabidi mzowee majaribu hayo.
Nani aliwaambia Vitambulisho vya Taifa vinatoka kwa Ubara na Uzanzibari?
Kinachotakiwa ni uhakika wa Uraia wa mtu, mpaka Wageni wanapatiwa kama wana vigezo vya kuishi kihalali nchini!
Wasiotaka Muungano Nyuso zimewaparama na makoo yamewafura!
ReplyDeleteMtajaza makoromeo pumzi kama vinyonga na nyoka vifutu lakini ng'ooo Muungano hautavunjika!
Nani aliwadanganya ya kuwa mtaimarika Kimaisha na Kiuchumi kwa kujitenga?
Dunia nzima, Wana Uchumi wanaamini ya kuwa matatizo ya kihali yanatatuliwa na Muungano wa Kiuchumi na Kinchi!
Hebu fungukeni akili zenu, mfano Sudani ya Kusini (Jubba) ilidai Uhuru kutoka Sudan (Khartoum), ikapatiwa Uhuru wake tarehe 11 Julai, 2011, lakini Mwaka huo huo tarehe 5 Desemba, 2011 Sudan (Khartoum) ikaomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mahsariki (EAC) huku wiki mbili baadae tarehe 19 Desemba, 2011 nayo Sudan ya Kusini (Jubba) ikaomba kujiunga na EAC!
-----------------------------------
ELEWENI KUWEPO KTK INTEGRATION (JUMUIYA YA NCHI) MAANA YAKE NI KUUNGNISHA UTENDAJI WA SERIKALI ZA NCHI HUSIKA KWA WIZARA ZOTE NYETI KAMA UCHUMI, SIASA, JAMII, ULINZI UTAWALA NA MIPANGO.
-----------------------------------
Kwa hivyo unaweza kuomba kujitenga lakini ukajikuta unatafuta MUUNGANO TENA KUTOKANA NA MAHITAJI YA KIUTAWALA UENDESHAJI WA SERILKALI NA UKUZAJI, KAMA ILIVYOWATOKEA SUDAN YA KUSINI NA SUDANI.
Kwa hivyo Vingozi wa Visiwani akili zao ni nzuri wameona mbali kwa hilo!
Wazanzibari jaribuni kufunguka mtoe ushirikiano ktk suala hili, kwa kuwa hata kama mtatawaliwa na Nabii gani hawezi kufanya Muujiza ktk Utawala wake wa Serikali atakayo iendesha bila KUWA NA WOWOTE MUUNGANO.
hahahahah Zanzibar itakuwa hakutoshi!
ReplyDeleteItakuwa hata kuagiza urojo pale Magenge ya Darajani unatakiwa utoe Kitambulisho cha Taifa!
Zanzibar,
ReplyDeleteChukueni Vitambulisho vya Taifa,
Mnaopinga Muungano mioyo imewajaa pumzi kibao!
Mtachukia mtapasuka Muungano DAIMA!, Mapinduzi DAIMA!
Safari hii Muungano ni kama TSUNAMI unataka hutaki utakokotwa na upepo!
Ohooo leteni ubishi mmezwe na Mamba ama kuangukiwa na NYUNDO YA CHUMA YA CHAMA CHA MAPINDUZI!
Suala la Vitambulisho vya Taifa na Muungano ni kama Mvua ya Gharika.
ReplyDeleteUkipanda juu ya paa la nyumba au bati, haisaidii!
Ukishika mizizi ya shina la mti haisaidii!
Ukikimbia kasi yako inazidiwa na maji ya gharika!
Wapinga Muungano itawauma saaana lakini ndio hivyo hakuna jinsi.
Na sasa Visiwani ndio mnashiriki Muungano kamili kuliko ilivyokuwa kabla.
ReplyDeleteZile kadi zenu za 'Ukazi wa Zanzibar' hazina viwango mtaweka darini ama kibindoni!
Mtoa Maoni wa 8 juu anony Fri Feb 15, 11:49:00 am 2013
ReplyDeleteGHARIKA LA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZENJI:
-----------------------------------
Ukipanda juu ya paa la nyumba au bati, haisaidii!
Ukishika mizizi ya shina la mti haisaidii!
Ukikimbia kasi yako inazidiwa na maji ya gharika!
-----------------------------------
1.UKIPANDA JUU YA PAA LA NYUMBA AU BATI,,,UNAKUTANA USO KWA USO NA MAMBA AU CHATU NAYE ANATAPA TAPA KUJIOKOA (KILA MMOJA ANAJIHANGAIKIA AJINUSURU NA ZAHMA) !
2.UKISHIKA MIZIZI YA SHINA LA MTI, NDIO KWANZA LINANG'OKA MNAKWENDA WOTE NA MAJI !
3.UKIKIMBIA KASI YAKO INAZIDIWA NA MAJI , NI BORA KUSALIMU AMRI NA KUKUBALIANA NA MUUNGANO NDIO NJIA PEKEE!
Si mchezo kamasi na jasho zinawavuja Wapinga Mapinduzi na Muungano!
Ama kweli Wabishi woooote Kimya!
ReplyDeleteHakuna cha Uanguko (uamsho), wala Wala wapinga Maendeleo, wala wapinga Mapinduzi, Wala Wapinga Muungano.
Sio mchezo,
-SERIKALI KIONGOZI!
-SERIKALI DUME!
-SERIKALI BABA!
Ili kudumisha Muungano na pia kuwawezesha Wapinga Muungano kuzoea hali ambayo inawabidi kuikubali,
ReplyDelete1.Utaratibu huu wa mchanganyiko uendelee, watu wa Uamsho na Magenge na Makundi ya Wapinga Muungano wapatiwe Vitambilisho vyao (BARA) huko Kwimba-Mwanza, Ludewa-Iringa,Kaliuwa-Tabora,Malampaka-Shinganya na Tarime-Musoma(kwa Wakurya Watani wao wanaofika Kisiwani kwa Operesheni mbali mbali wakiwa Vikosini) !
2.Wengine Bara Wakurya na Waryanchoka wa Tarime na Rorya-Musoma, na wale wa Buseresere-geita walikofanya mapigano wakachukulie Vitambulisho vyao vya Taifa huko (VISIWANI) Zanzibar na Pemba!
Hivyo nanyi Wakurya kutoka Bara muweze kuonana na Watani zenu Visiwani, huku kwa mara ya kwanza, mkiweza kuiona Bahari na mkisafiri Baharini kwa vyombo vya bahari.
HII NDIO RAHA YA UNDUGU WA MUUNGANO!
Ahsante sana Serikali kwa uamuzi na mpango wa utoaji vitambulisho huu wa busara sana!
Yule Mzanzibar Mpinga Muungano na Wafuasi wake vipi upo Likizo?
ReplyDeleteHehehe hadi vidole vimekufa ganzi huwezi kabisa kupiga keyboard za Laptop yako kutuma Maoni!
;;;;;;;;;;;;;;;;
Assalam Alaykum!
Ukubwa ni jiwe lazima ukubali kushindwa licha ya jazba na majigambo yako na ubishi wako!!!
Je, unaona kazi ya kugawa Vitambulisho huko Zenj inaendelea kama unavyoona!
Lazima wewe na wafuasi wako mjifunze kuiheshimu Serikali.
Kwa kweli joto limepanda sana, au umesha chukua cha kwako tayari?
Mpinga Muungano Mzanzibari vipi na genge lako?
ReplyDeleteAu mpo Likizo?
Wapinga Muungano eeeeee!
ReplyDeleteSerikali hiyooo!
Serikali hiyooo!
Serikali hiyooo!
Inakuja kugawa Vitambulisho vya Taifaaa!!!
...................................
trrrrrrr wanakimbia mara eee Ukuta Mkubwa mbele hakuna pa kupita!
Ohhh Makeme ukuta mbeleni tufanyeje?
Makame anajibu:HATUNA JINSI TUPANGE FOLENI TUPEWE VITAMBULISHO!
Wapinga Muungano harakati zenu dhidi ya Serikali ni sawa na kupiga ngumi ukuta!
ReplyDelete,,,mara mkono poooo umevunjika!
Matokeo yake unakuta unawahishwa Hospitalini Mnazi Mmmoja Zanzibar!
Mwana Mapinduzi nasema Assalam Alaykum Wapinga Muungano!
ReplyDeleteNa sasa NSSF imetua hapo Visiwani huku ZSSF ikitakiwa nayo ichanue mwabwa zake hadi Bara!