Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)moja ya silaha walizokamatwa nazo watuhumiwa .
Waaandishi wa habari wa Mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza maelezo toka kwa kamanda wa polisi wa mkoa huo Robert Boaz(hayukopichani).
Baadhi ya viongozi waandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

JESHI la polisi mkoani kilimanjaro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Robert Boaz amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Mohammed Shani (24) na Emmanuel Jumanne (30), wote wakazi wa Bomangombe na Sanya juu wilayani Hai.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda Boaz amesema kuwa januari 19 mwaka huu majira ya saa kumi jioni huko Bomangombe mtuhumiwa wa kwanza Mohammed Shani alikamatwa akituhumiwa kujihusisha na matukio mbali mbali ya unyanganyi kwa kutumia silaha.

Boaz amesema mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikiri kuwa anayo silaha ambayo huitumia kwenye matukio mbali mbali ya uhalifu akiwa anashirikiana na wenzake ambapo aliweza kuwaonyesha polisi sehemu alipokuwa ameihifadhi silaha hiyo.

Kamanda Boaz, amesema kuwa silaha iliyokutwa na mtuhumiwa huyo ni, Bunduki aina ya MARK IV ambayo imefutwa namba za usajili na kukatwa kitako na mtutu pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu kama kinyago (mask) 1,maboshore 2, masweta 2,pamoja na risasi 13.

Kamanda Boaz, amesema baada ya kuhojiwa, Mtuhumiwa alimtaja alimtaja mtuhumiwa wa pili Emanuel Jumanne na kuelekeza chumba anamoishi na kilipopekuliwa ilipatikana bunduki moja aina ya shortgun iliyotengenezwa kienyeji na risasi mbili za shortgun, kofia ya jeshi la polisi, boshore 1,begi dogo lililokuwa limehifadhia bunduki hiyo.

Aidha kamanda aliongeza kuwa msako ulianza na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa wilayani Karatu ambapo kwa pamoja walikiri kufanya matukio mbali mbali katika maeneo ya Bomangombe na Sanya juu na Moshi.

Boaz aliongeza kuwa makosa mengine ni madereva wasiokuwa na leseni,ulevi,kutokuwa na motor vehicle licence,kutokuwa na bima na kupakia abiria kwenye magari ya mizigo.

Amesema kiasi hicho cha fedha kimetokana na tozo za notification na lengo kuu likiwa ni kupunguza ajali za vifo na majeruhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...