Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waaandishi wa habari (hawapo pichani) madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokuwa kwenye moja ya viroba kati ya 20 vilivyokamatwa na Polisi,mkoa Arusha.
MNAMO TAREHE 31/01/2013 MUDA WA SAA 7:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LOSOITI KIJIJI CHA KIMOKUWA WILAYANI LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA ASKARI MGAMBO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA AITWAYE MANDEGE S/O PAKASI (54) MFUGAJI NA NI MKAZI WA KITONGOJI CHA LOSOITI AKIWA NA MAGUNIA 20 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI YANAYOKADIRIWA KUWA NA UZITO WA KILOGRAMU 50 KILA MOJA.
TUKIO HILO LILITOKEA MARA BAAADA YA ASKARI HAO KUPATA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA, AMBAPO INAELEZWA KWAMBA MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA WENZAKE WAWILI WALIKUWA WANASAFIRISHA MADAWA HAYO KWA KUTUMIA WANYAMA AINA YA PUNDA AMBAO WALIKUWA KUMI AMBAPO KILA MMOJA ALIKUWA AMEBEBESHWA MAGUNIA MAWILI.
MARA BAADA YA WATU HAO KUWAONA ASKARI HAO WATUHUMIWA WAWILI WALIKIMBIA NA WAKAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA MMOJA.
JESHI LA POLISI MKOANI HAPA BADO LINAENDELEA KUMHOJI MTUHUMIWA HUYO HUKU WATUHUMIWA WAWILI WALIOKIMBIA WANAENDELEA KUTAFUTWA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
Yaani nashangaa sana! Wanaovuta bangi ni wale wenye vipato vya chini na ina soko si mchezo. Watu wanatajirika kwa kuwamaliza maskini! Kazi tunayo!
ReplyDeleteMajani ni mboga na majani pia ni dawa!
ReplyDeleteKiongozi Kamanda Mkuu wa Usalama wa Mkoa pongezi kwa kazi isipokuwa, zaidi ya mabangi na mirungi mnayokamata muangalie pia klitu hatari zaidi ambayo ni Unga!
Kamanda kazi ni nzuri Hongera,
ReplyDeleteIsipokuwa pana Miswaada mingine nyeti zaidi Kuisalama hapo kwako Arusha,
1.Pana haya Makundi ya Watu wanaoitumia Siasa kufanya Uhalifu, na Ujambazi.
2.Pana hawa Wachimba madini ambao sijui wamefilisika au wameshindwa kujiendesha, wanasumbua sana kwa matukio kama Mauaji,Uporaji, Uvunjaji wa Sheria za nchi na kila aina ya Uhalifu huku wakikingiwa vifua na wakishirikiana na Wanasiasa (sitaji Chama husika, naweka kapuni).
3.Wengi ni kuwa wanshindwa kutofautisha kati ya 'Upinzani wa Kisiasa na Uvunjaji wa Sheria za nchi'
Arusha ni 'image'/taswira ya nchi na Eneo la Afrika ya Mashariki kwa ujumla, kwa kuwa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki huku Mhe.Balozi Dr. Richard Sezibera Katibu Mkuu wa Jumuiya akiwa ndio Makazi yake...Pia ni Eneo letu Muhimu Kiuchumi kwa Mapato ya Sekta ya Utalii.
Hayo matatu (3) ni mambo nyeti sana zaidi ya 'mabangi' na 'mirungi' Kimkoa na kwa Ustawi na Usalama wa Nchi ya kuyashughulikia mezani kwako wewe pamoja na Vikosi vyako vya Vijana wako wa kazi.
ReplyDelete"Majani ni mboga, majani pia ni Dawa" KWELI 100%
Viwango vya uteja (addiction rates) from scientific research.
1. Sigara
2. Pombe
3. Unga
4. Kahawa
5. Bangi
Bangi is less addictive, BELOW Coffee!
Marekani-
Idadi ya vifo kutokana na Sigara, watu laki 4 kwa mwaka.
Vifo kutokana na uvutaji wa Bangi? ZERO. Uchunguzi umekuta HAKUNA vifo vinavyotokana na uvutaji wa Bangi.
Bangi ni majani, unaweza kuacha muda wowote na kusiwe na athari zozote.
Mwaka 1883 rudi nyuma miaka elfu moja Bangi haikuwa haramu. Na ilikuwa ni zao KUBWA kabisa la BIASHARA.
Waliohusika kuiharamisha, walikuwa na mkono kwenye biashara ya magogo (karatasi). Siasa ikaingia.
Kuharamisha kwake hadithi yake ni ndefu sana, huko nyuma haikuwa haramu kwani iko na matumizi mengi SANA.
1. BIOFUEL, kuna gari ilitengenezwa inatumia mafuta yatokanayo na Bangi. Mvumbuzi akauawa.
2. Kamba ngumu sana.
3. Saruji (hempcrete)
4. Vitambaa imara SANA, ugumu wake ukiwa ni mara tano zaidi ya vitambaa vya pamba
5. Karatasi imara SANA
6. Dawa
HADITHI NI NDEFU SANA.