Waziri wa Habari, Vijana ,UtamaduninaMichezoDkt. Fenella Mukangara akifungua mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwasilisha mada kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa HesabuzaSerikali Sarah Reuben akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka Iringa Bw. Majjid Mjengwa akitoa mda kwa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa mawasiliano serikalini mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao kazi hicho mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi mwenyekiti Mjengwa na washiriki wengine kwa semina hii.

    ReplyDelete
  2. Nimekuona Grace "tha boss" wakilisha NHIF mamaaaa!
    Nani kanunaaaaaa.........!???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...