Habari na picha na John Nditi, Morogoro
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi ameliomba Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kutoa wataalamu wa kufanya uchunguzi wa kina juu ya mifumo ya maji machafu wenye kemikali yanayotililishwa katika mto Ngerengere kutoka katika baadhi ya viwanda ili kuwanusuru wakazi wa Morogoro.
Pia ameiomba Wizara ya Malisili na Utalii kutoa wataalamu wasaidia kufanya kazi ya kudhibitisha magogo yanayotumiwa na kiwanda cha nguo cha 21st Century yanavunjwa ipo na iwapo ni kwa njia halali ili kubainisha hatua za kuchukuliwa za kudhibiti uvunaji wa magogo.
Mkuu huyo wa Wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alitoa ombi hilo Februari 20, mwaka huu kwenye majumuisho mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Ngozi ‘Tannery’ Morogoro na kiwanda cha nguo cha 21st Century cha Morogoro.
Ziara hiyo ya ghafla katika viwanda hivyo ni utekelezaji wa maagizo ya wadau na wananchi Wilaya ya Morogoro katika kikao cha ushauri cha Maendeleo ya Wilaya ya Morogoro ( DCC) . Mkuu wa Wilaya alisema hayo mbele ya Meneja Uzalishaji wa Kiwanda hicho, Clementi Munisi,ambapo licha ya kuupongeza uongozi wa kiwanda kwa baadhi ya mambo mazuri , lakini pia alikerwa kuona kiwanda hicho kimekuwa ni kichocheo cha uharibifu wa mazingira ya ukataji wa miti ya asili.
“ Kwa mambo mazuri nmanyoyafanya tunawapongeza, lakini hatukubaliani na suala la ukataji wa miti ya asili , na tumejionea wenyewe magogo yaliyorundikwa ni ya miti ya asili tofauti na kauli uliyotuambia ya asilimia 95 ni miti ya kupandwa” alisema kwa masikitiko Mkuu wa Wilaya.
Serikali ya Wilaya haijaridhishwa kuona hali hii ya ukataji wa miti tena marundo haya sehemu kubwa ni miti ya asili na sasa tutaanza kuchukua hatua kwa kutumia vyombo vyetu” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
“ Najua wapo wengi walioshindwa juu ya jambo hili, lakini hatutaacha kupinga kelele ikibidi tutafika mbali , hatuwezi kuona watu wa Morogoro wanakosa mvua kutokana na uharibifu wa mazingiora hasa unaochochewa na kiwanda “ alisisitiza Mkuu wa Wilaya .
Hivyo alisema , licha ya mchango wa Viwanda hivyo katika kukuza uchumi wa taifa na kuongeza vipato vya Watanzania , vinapaswa kutunza afya za wananchi na mifugo kwa kuboresha mazingira na kutumia nishati mbadala.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Ande Malango, ambaye ni Ofisa Misitu na Maliasili wa Wilaya hiyo, alisema kuwa asilimia 98 ya magogo yaliyohifadhiwa ndani ya Kiwanda yanatokana na miti ya asili jambo ambalo ni kwenda kinyume na sheria za nchi.
“ Hata ni asilimia mbili tu tunaweza kusema tumeona magogo ya miti ya kupandwa ya aina ya saligina na Citriodora na iliyobakia ni ming’ongo, mining’a poli , miyegea na miyombo ambayo ni miti ya asili iliyokaatwa na kuchanganywa na hii ya kupanda” alisema Malango.
Akifafanua baadhi ya shituma dhidi ya Kiwanda hicho, Meneja wa Uzalishaji wa Kiwanda , Munisi, alisema kwa asilimia kubwa kiwanda kinatibu kwa dawa maji wenye kemikali yanayotoka kiwandani kabla ya kutililishwa mtoni na kuwaondolea hofu wananchi kuwa maji yanye rangi hayana madhara.
Meneja Uzalishaji huyo pia alisema , Kiwanda kinatumia asilimia 95 ya kuni zitokanazo na magogo ya miti yanayolewa na wafanyabiashara wenye leseni kutoka mamkala husika na idadi kuwa ni kutoka mkoa wa Iringa na asilimia tano ni miti ya kawaida ni kutoka mkoani Morogoro .
Hata hivyo alikiri kuwa , Kiwanda kimekuwa kikitumia magogo kwa kununua kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni zinazotolewa na mamkala husika kwa ajili ya kuendeshea mitambo na pia umeme kwenye mashine , ambapo alisisitiza kwa kusema endapo gesi itafikishwa mkoani Morogogro kiwanda kitaondokana na matumizi ya kuni.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Ande Malango , ambaye ni Ofisa Maliasili na Misitu wa Halmashauri hiyo akipita juu ya vipande vya magogo ya miti iliyokuwa imehifadhiwa ndani ya kiwanda cha 21st Century Textiles kilichopo eneo la Kihonda, Manispaa ya Morogoro, Kiwanda hicho kinanunua kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya mkoa kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ‘ Boiler’ za kuchemshia maji, kitendo kinacholalamikiwa na wananchi kuwa kunachangia uharibifu mkubwa wa mazingira ya ukataji wa miti ya asili ovyo.
Matumizi ya kuni kuendeshea mitambo ya kiwanda ilivyokuwa ni kichocheo cha ukataji wa miti ya asili ndani na nje ya Mkoa wa Morogoro, kama vipande vya magogo ya miti vilivyokutwa ndani ya eneo la Kiwanda .
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakipinga picha sehemu ya rundo la vipande vya magogo ya miti vilivyohifadhiwa ndani ya kiwanda cha 21st Century Textiles eneo la Kihonda, Manispaa ya Morogoro, kiwanda hicho kinanunua kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya mkoa kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ‘ Boiler’ za kuchemshia maji, uamuzi ambao unalalamikiwa na wananchi kuwa kinachangia uharibifu mkubwa wa mazingira ya ukaji wa miti ya asili ovyo
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Nguo cha Morogoro, Clementi Munisi mbele wakimwongoza DC Said Amanzi (wapili )anayemfuatia kuelekea kwenye mabawa ya kutibu maji machafu
Gari lilolobeba shehena na vipande vya magogo ya miti likiwasili kiwandani kama lilivyokutwa nje ya lango kuu

Huu ni Usanii sasa kwa upande wetu Viongozi. Kiwanda hiki si mara ya kwanza kutembelewa na kushutumiwa na ufisadi wa maliasili!
ReplyDeleteYaani hata vipande vya Mpingo vinaonekana ktkt ya "kuni" hizi. Tusishangae! Viongozi chukueni hatua madhubuti na endelevu
21st Century Textiles? au ni 12th Century Textiles?
ReplyDeleteNadhani mbadilishe jina tafadhali, kwa sababu hamstahili kuitwa wa Karne ya 21 kwa kuwa bado mpo Karne ya 12 kwa kuharibu Mazingira!!!
Hivi mmeshindwa hata kutumia lalternative Green Energy kupata uwezo wa kuendesha kiwanda?
Kwa nini msitumie kati ya hizi:
-Solar power
-Geothermal
-Wind energy
???
Hiyo ni 18th Century technology badala ya 21st Century.. Shame!!!!
ReplyDeleteHicho kiwanda kifungwe haraka. Watumie makaa ya mawe kwa nishati.
ReplyDeleteHakika huu ni uharibifu wa mazingira. Viongozi Kataeni uwekezaji huu wa madhara kwa misitu na mazingira yetu na chukueni hatua. Serikali kuu iwalinde viongozi wa mkoa na Wilaya.
ReplyDeleteNdugu Michuzi,
ReplyDeleteNashukru sana ka kurusha hili janga la taifa na kiashiria cha rushwa kubwa.Mimi ni mkazi wa morogoro-kusema kweli hawa wenye hiki kiwanda Magogo hawayanunui toka kwa wafanyabiashara.Ushaidi ninao hawa jamaa wamemaliza miti inayoota kando ya mito na hasa maeneo mengi ya Morogoro na kuanzia na maeneo ya Mlali,Kipera ambako nilishuhudia wakikakta miti nya Poli ambayo imekuwako kwa miaka mingi na ilikuwa mikubwa sana.Kinachosikitisha na nkunialzimu kusema kuna rushwa na pia janga--Kuna viongozi wa vijiji kwa umaskini wao wanapewa pesa ndogo kisha kuruhusu miti ikatwe bila huruma.Pia nina omba uchunguzi ufanyike wa kina Kuna hujuma kwa kuruhusu kiwanda hicho-Nina wasiwasi kuna wahusika toka ngazi kubwa zote zinazohusika na mazingira na hao either wana masrahi ya kupewa pesa au kushinikizwa na walipewa pesa.
Haiwezekani karne ya 21 unaleta kiwanda cha kuni halafu unaita 21 century--ni nchi gani unaweza kukuta kiwanda kama hicho.Hao jamaa wawaonyeshe wahusika recods za malipo ya magogo na wajue nani anauza na msitu wake uko wapi.
Kwa morogo hao wamezidi hadi wakata mkaa.KIWANDA HICHO NI CHA KUOGOPA KAMA UKIMWI NA UKOMA.
mAGARI YANAYOBEBA MAGOGO YANAPITA YAMEFUNKIWA ILI KUFICHA YAMEBEBA NINI.
Ukikutana nalo ni vigumu kujua kama kweli limebeba magogo.
NARUDI USHAHIDI NINAO KUWA ZAIDI YA 50& YA MAGOGO YEMEVUNWA NDANI YA MVOMERO,MOROGORO VIJIJINI,MOROGORO MJINI NA NI MITI YA KANDO YA MITO NA SI YA KUNUNUA TOKA MASHAMBA YA MITI.
WASEME MSTU GANI WANANUNUA HAYO MAGOGO-NA WATAALMU WA MITI WAYAKAGUE KUONA KAMA KWELI NI MITI YA ASILI AU KUPANDA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU WALAANI WANAOANGAMIZA KIZIZI HIKI NA KIIJACHO CHA NCHI YETU.
kiwanda hicho kina harufu mbaya ya rushwa na ushahidi ninao kuwa magogo hayo kwa zidi 50% ni miti ya asili na naweza kuwapeleka sehemu nyimgi ambazoyamekatwa maeneo ya mvomero--Kipera,Malalli.Hata hivyo hawa jamaa huzunguka sehemu nyingi na hubeba magogo hayo kwa gari kubwa na huficha wakati wanasafirisha.
ReplyDeleteMnao wataalu wa miti hapo SUA,wapelekni wachunguze-mtanona miti hiyo si kupanda ni miti ya asili na imekuwepo kwa miaka mingi.
Ila viongozi wa vijij wanapokea pesa kwa umaskini wao wanaruhusu ikatwe.
Na kuna uwezekano mkubwa kiwanda kina mkono wa watu toka Agency za serikali zinazohusika hivyo kuwahusha washukíwa-hakutaleta matunda yoyote.Ni aibu karne ya 21 kuwa na kiwanda cha kuni na mtu huyo hana msitu na wala hachangii hata kuendeleza mistu nchini.
JAMANI MNATUPELEKA WAPI?? WANAOHUSIKA KAMA MPO FANYENI KAZI HII NI RUSHWA KUBWA PCCB AMUKENI--KIWANDA HIKI KINA HARUSU YA RUSHWA TOKA WIZARA HUSIKA,MKOANI,WILAYANI,HADI KWA VIONGOZI WA VIJIJI.
No , for God's sake , this must be stopped immediately!Hiki Kiwanda kinakwepa gharama kubwa za Umeme , lakini, kina ua mabisa mazingira yetu,hilo halitakubalika!Serikali itapaswa kutafuta kiini cha tatizo hilo,na sio kukurupuka tu kwa kuwalaumu wenye Kiwanda!Tunataka kiwanda kiendelee kuzalisha ili kulinda ajira za watu na kutengeneza faida kwa Taifa,lakini wakati huohuo, uharibifu wa mazingira lazima ukomeshwe kabisa!Serikali, Tanesco na Menejimenti ya Kiwanda wakae pamoja na kutafuta suluhu!La sivyo,nguo zitakazo zalishwa hapo kiwandani hazita nunulika kutokana na bei kubwa kuliko ile ya ushindani!nafikiri nime eleweka!
ReplyDeleteJina la kiwanda haliendani hata chembe na ukweli eti "21st CENTURY TEXTILE LTD"
ReplyDeleteTatizo letu WaTz tunapenda sana ziara hizi ambazo zina ambatana na Posho. Subiri tuone kama kiwanda hiki hakitakuwepo mwisho wa mwaka huu 2013 kikiwa kimeteketeza tani 5000 za magogo. Hapendwi mtu Pochi!
ReplyDeleteInasikitisha sana sana Hiki ni moja wapo ya viwanda vya Mohamedi Enterprise group. Moja wa wamiliki wake ni Mbunge wa Singida kupitia CCM Bwana Mohamed Enterprise. Na anablog yake inaitwa MOBLOGSPORT.
ReplyDeletePls michizi hizi picha na maoni yetu mpelekee aone jinsi viwanda vyake vinavyoharibu uwai wa kizazi kichacho. Shemi on you Mohamed Dewji na kundi lako.
Hapa tunaingizwa mjini, ndiyo maana pale Gairo magari yanapita kila siku yamejaza magogo mengi.
ReplyDeleteSERIKALI IKO WAPI JAMANI??????????????????
Hivi niwaulize enyi 21st Century Textiles na hao Viongozi wa Mamlaka hapo Morogoro je thamani ya majora yenu mnayozalisha ya nguo yanalingana na thamani ya Mazingira asilia?
ReplyDeleteThink twice and decide!
21st Century Textiles mmekuwa wazito sana wa kufikiri!!!
ReplyDeleteHapo hapo Morogoro pana Viwanda vya Miwa na Sukari kibao Mkoa mzima, Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar mnatakiwa mtumie muwe High tech Innovations:
Tatizo biashara nyingi hazialiki wataalamu ktk hatua ya Mipango (Business Developement stage) na mambo maengi yanaendeshwa Ki-mjomba mjomba nchini Tanzania.
PANA NJIA MBILI AMBAZO NI ENDELEVU(SUSTAINABLE SOLUTIONS)hapa chini:
1.'Bio-Ethanol Energy' (baada ya miwa kukamuliwa pana layer ya mafuta juu ya juice ya maji ya miwa inazalisha energy nyingi sana) hii inaenguliwa kutoka kwenye juice kwa tekinolojia ya chujio maalum na kujazwa kwenye Mapipa na Mitungi kwa kwenda kuzalisha Nishati.
2.'Methane energy' kwa makapi ya miwa, ambayo yamesha kamuliwa yanatoa kiwango kikubwa sana cha Energy yakichomwa.
Nchi kama Mauritius zina Kampuni amabzo zinazalisha vinu vya kubadili Ethanol waste kuwa nishati kamili pia vipo vinu vya kuchomea Methane waste ili kuzalisha Nishati.