![]() |
MAREHEMU NAZARETH MWAMGOGWA |
NI MIAKA 25 SASA IMEPITA TANGU ULIPOTUTOKA RASMI HAPO TAR 06-02-1988.SISI WANAO ISAAC,SUMA,IMMA NA REBECCA.
TUNAKUKUMBUKA DAIMA.KWA MAJONZI TULIYOKUWA NAYO ULIPOTUACHA GHAFLA KWA AJALI HATUKUDHANI KAMA ITAFIKA SIKU KAMA YA LEO IKIWA NI MIAKA 25 IMEPITA TUKIWA WOTE BADO HAI.KWA UWEZA WA MWENYEZI MUNGU WOTE BADO TUKO HAI NA AFYA NJEMA.NAFASI YAKO MIOYONI MWETU ITAENDELEA KUWEPO MPAKA HAPO TUTAKAPOKUTANA TENA.UTAENDELEA KUKUMBUKWA KWA UCHESHI WAKO NA UNADHIFU WAKO BILA KUSAHAU NGUVU ZAKO KATIKA KUSIMAMIA HOJA UNAYOIAMINI.
WANAO BADO TUNAENDELEA NA TUTAENDELEA KUSIMAMIA UKWELI NA KUSAHIHISHA PALE TUNAPOONA HAPAENDI SAWA.
UNAKUMBUKWA NA NDUGU WOTE SIKU ZOTE HASA MAMA YAKO TUKUSUMA MWAKINGWE,WADOGO ZAKO ELLY NA RUBEN,BILA KUSAHAU WANAO WENGINE BARAKA NA TULLY.
TUNAENDELEA KUKUOMBEA KWA MUNGU AKUPE MAISHA MEMA NA YA AMANI HUKO ULIKO MPAKA HAPO TUTAPOONANA TENA
MUNGU AILAZE ROHO YAKO PEMA.AMEN
R.I.P.BABA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...