
Ilikuwa ni siku iliyojaa simanzi kwa mume wako kipenzi Abdallah, watoto wako Hashim na Lulu, mama yako mzazi Mama Babay, Baba yako mzazi Mzee Abdul, kaka yako Yusuf, wadogo zako, shangazi na baba zako wadogo, ambao bado wanakukumbuka.
Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena. Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja, viungo vitaungana tena.
Mungu ametimiza ahadi na mapenzi yake ya kukuita kwenye makazi yake ya kudumu ukapumzike kwa amani, baada ya kuishi nasi duniani kwa furaha, ukarimu, amani na upendo kwa miaka 42. Kimwili haupo nasi nyumbani, lakini ki roho bado uko nasi popote.
Ni mwaka mmoja kamili umetimia leo, lakini kumbukumbu za upole, ukarimu na tabasamu lako, zinatufanya tuone kama umeondoka jana. Dua njema tunakuombea, Mwenyezi Mungu alijalie kaburi lako liwe miongoni mwa bustani za peponi.
Daima unakumbukwa pia na shemeji zako Dawood, Shigongo, Nasibu, Hassan, Kitenge, wafanyakazi wote wa Global Publishers, wifi zako, majirani na marafiki zako wote.
Kifo chako kinaendelea kutukumbusha kwamba kila nafsi itaonja mauti na ulipoiaga dunia tulisema:
HAKIKA WEWE NA SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE SOTE TUTAREJEA! UWEZO NA UTUKUFU WAKE UTUKUZWE DAIMA - AMIIN!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...