ROSE KAPYA MWAILENGE

Ilikuwa saa 11.00 jioni, siku kama ya leo tarehe 27 February, 2006 ulipotutoka. Wakati bado tulikuhitaji sana, tulidhani ni ndoto tu.Japo sote tuliamini kuwa siku moja ungeamka ukiwa mzima.Mama,japo leo ni miaka saba tangu ututoke,bado tunahisi tuko ndotoni na tumeshindwa kabisa kukubaliana na ukweli kwamba haupo nasi. Mara kwa mara nakuona ndotoni, lakini ninapoamka nagundua ni ndoto tu,na hiyo inazidisha uchungu na majonzi.

Japo siku zote tangu ututoke tumekuwa na wakati mgumu sana ,siku hii ya leo tunapoadhimisha miaka saba ya kifo chako ni ngumu zaidi kwetu.Inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.
  
Kazi ya Mungu haina makosa.Tukijiuliza sana kwanini alikuchukua wakati bado tunakuhitaji sana tutakuwa tunakufuru.Tunajaribu kujifariji kwa kuamini kuwa alikuchukua kwa vile alikupenda zaidi yetu.Na tunajitahidi pia kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani na unaangaziwa mwanga wa milele ukistarehe kwa amani.Japo haupo nasi kimwili lakini siku zote tupo nawe kiroho

Unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa Bupe, Lilian na Shirima, Fred na Furaha bila kuwasahau wajukuu zako Irene-Kanyampa, Aziz-Elian, Rose, Junior-Ereneus na Katarina.


Pumziko la Milele Akupe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Akuangazie Ustarehe Kwa Amani,  AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...